Showing posts with label Linnah. Show all posts
Showing posts with label Linnah. Show all posts

Linah Sanga: Natamani Kutoka Kimapenzi na Wizkid

Akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana (EATV) Linah Sanga alisema kuwa toka kipindi cha nyuma alikuwa anatamani kuwa na msanii huyo kama mpenzi wake, ingawa anadai mpaka sasa ndoto yake hiyo haijaweza kukamilika mpaka dakika hii.
"Unajua nilikuwa namu admire Wizkid toka muda mrefu, na ndiyo mwanaume ambaye hata ukiniuliza ni msanii gani wa kiume katika bara la Afrika ambaye ungependa kuwa naye au ambaye nampenda nitakwambia ni Wizkid, siwezi kukataa ila ndiyo hivyo tena maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli" alisema Linah Sanga.
Katika hatua nyingine msanii huyo kwa sasa anasema ameamua kufanya tu kazi na kuachana na masuala ya mapenzi na kusema kuwa akichanganya kazi na mapenzi mwisho wa siku hata kazi yenyewe anaweza kuharibu.

Linah amedai mpaka sasa ana mipango ya kufanya kazi na Wizkid ingawa anadai kwa sasa alimwambia yupo 'busy' kidogo mpaka siku za usoni ndipo wanaweza kukamilisha kazi hiyo.

Ukweli wa Linah kuhusiana na Tuhuma za Kutoa Rushwa ya Ngono

Kipindi cha Enews kinachorushwa na East Africa Television kilitaka kufahamu kama kuna ukweli wasanii hao wa kike huhonga ngono ili wafanyiwe kazi nzuri kwenye hizo kampuni kubwa, Linah Sanga ambaye hata yeye amefanikiwa kufanya videos na waongozaji wakubwa wa video barani Afrika akiwepo Godfather alikuwa na haya ya kusema.
"Sijui kama ipo hivyo sababu mimi kama msanii wa kike sijawahi kufanya kitu kama hicho, kwa hiyo sidhani kama hicho kitu ni cha kweli kwa sababu ukifuatilia kwa wasanii wakubwa wa kike ambao tumeweza kufanya kazi na madirectors wakubwa kama God Father na wengine ni mimi, Vanessa, labda na Aika kwa sasa hivi ambao tayari tumeshatoa kazi zetu, kwa hiyo sidhani kama hicho kitu ni kweli kwa sababu tunafanya kazi na kazi zinalipa ndiyo maana tunaweza kufanya kazi na watayarishaji wakubwa kama hivyo". Alisema Linah Sanga.

MAHABA NIUWE!!!Mpenzi mpya wa Linnah ajichora "tattoo" ya jina la Linnah kwenye mwili wake


Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi aitwaye,Nagari,Staa wa Bongo Fleva,Linnah Sanga amepata mpenzi mpya aitwaye Williams Bugeme’Boss Mutoto’raia wa Uganda,ambaye hivi karibuni amechora ‘tattoo’ kwenye mwili wake yenye jina la msanii huyo. 
Akizungumza na Clouds FM,Linnah alisema ilikuwa ni kitu cha kushtukiza sana kwani mpenzi wake alimtumia sms kuwa anataka kumfanyia ‘surprise’ na afikirie ni kitu gani anataka kumfanyia alimjibu kuwa hajui ila amwambie tu. 
‘’Alinitumia sms akaniambia ni ‘guess’ ni kitu gani anataka kunifanyia ‘surprise’ nikwambia mimi sijui basi akaniambia amechora tattoo yenye jina langu daah! Nilishtuka sana na pia nilikuwa na furaha sana,’’alisema Linnah.
 ‘’Unajua ni maamuzi magumu sana mtu kukuchora tattoo na mpaka anakuchora ujue basi ana mapenzi ya kweli na kama ni shabiki basi ni shabiki kwelikweli amezama kabisa,’’aliongeza Linnah.
 Msanii mwingine aliyeweka rekodi ya kuchora tattoo ya jina la mpenzi wake na sura yake ni msanii wa Bongo Fleva,Nuh Mziwanda aliyechora tattoo ya mpenzi wake Shilole.