Showing posts with label Shilole. Show all posts
Showing posts with label Shilole. Show all posts

Hii Kali!SHILOLE adai bila Milioni 20 haumpati Kamwe!

Amepanda dau? Msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa bila mtu kuwa na kiasi cha Sh. Milioni 20 mkononi, hawezi kucheza filamu yake kwa kuwa kwa sasa anaona kama ni kumpotezea muda.

Akipiga na Ijumaa Wikienda, Shilole au Shishi Baby alifunguka kuwa soko la filamu Bongo, linashuka na pia wasanii wanatumia muda mwingi lakini wanapata malipo kidogo tofauti na nguvu pamoja na muda waliotumia.

“Kama mtu akinitaka kwa sasa ili nicheze filamu yake awe na milioni 20 ndiyo nifanye maana ni kitu ambacho kinachukua muda sana halafu malipo yake ni kidogo,” alisema Shilole.

Chanzo:GPL
Ni kweli Shilole amekahidi Adhabu aliyopewa na BASATA?Tazama picha alizopost Ommy Dimpoz na alichoandika...!

Ni kweli Shilole amekahidi Adhabu aliyopewa na BASATA?Tazama picha alizopost Ommy Dimpoz na alichoandika...!

Msaani wa Bongo fleva nchini Shilole ameondoka nchini kuelekea Marekani kufanya Show akiwa na Ommy Dimpoz. Katika picha aliyoipost Ommy Dimpoz zikiwaonyesha wameshuka katika Uwanja wa Ndege wa Houston nchini Marekani wakati huo huo Shilole akiwa bado anatumikia adhabu ya mwaka mmoja aliyopewa na Baraza la Sanaa nchini.
Katika Post hiyo Ommy Dimpoz ameandika 

'Touch Down Huoston Tx with Shishi beibee @shilolekiuno AMERICA wussup?!! See u this Saturday at club Safari'

Swali tunalojiuliza, Je? Shilole amesahamewa ile Adhabu au ameamua kukahidi hiyo adhabu ambayo ilimtaka hasijishughulishe na Muziki ndani na nje ya nchi kwa Muda wa Mwaka Mmoja.
BASATA:Adhabu ya Shilole ipo pale pale!

BASATA:Adhabu ya Shilole ipo pale pale!


Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetoa kauli kuwa adhabu ya kufungiwa kutojihusishwa na sanaa kwa mwaka mmoja ndani na nje ya nchi msanii Shilole ipo palepale, kauli ya hiyo imekuja baada ya msanii huyo kusema kuwa atakwenda kufanya shoo nchini Marekani pamoja na msanii mwenzake Ommy Dimpozi licha ya kufungiwa kwa mwaka mmoja.
Akiongea na East Afrika Radio Shilole alisema amejiandaa vizuri sana katika shoo ambayo anapaswa kuifanya nchini Marekani siku za karibuni, na alipoulizwa atawezaje kufanya shoo hiyo wakati akiwa amefungiwa na BASATA, Shilole alionekana kupaniki na kubadilika na kumwambia mtangazaji kuwa yeye hataki kuzungumzia suala la adhabu iliyotolewa na BASATA na kusema suala hilo anapaswa kuulizwa mwanasheria wake Albert Msando.
Hata hivyo kwa upande wa BASATA, Afisa Habari wa baraza hilo, Bw. Basyeibya amesema adhabu ya msanii huyo ipo palepale na wao wanaamini kwamba msanii Shilole anaitekeleza adhabu hiyo na
iwapo atakiuka adhabu hiyo watachukua hatua nyingine zaidi mbele.
"Adhabu ya Shilole iko wazi kwa maana ya kuzuiwa kufanya onyesho ndani na nje ya nchi utakumbuka kuwa kosa ambalo lilimfanya kufungiwa alilifanya nchini Ubelgiji kwa hiyo adhabu yake ipo pale pale haijatenguliwa hivyo hatakiwi kufanya onyesho lolote ndani au nje ya nchi, “alisema Bw. Basyeibya na kuongeza kuwa, “Kama anaweza kukiuka adhabu hiyo sisi Basata iwapo atakiuka adhabu hiyo tutachukua hatua zaidi dhidi yake".
Eatv.tv
Shilole: Wanataka nianze Kuiba Waume za Watu...Ila Nisilaumiwe!

Shilole: Wanataka nianze Kuiba Waume za Watu...Ila Nisilaumiwe!


Mwanamuziki wa miondoko ya mduara ambaye kwa hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kilichotolewa na  Baraza la Sanaa Basata  ya kutojihusisha na shughuli za kisanaa mpaka mwaka mmoja, kitu ambacho kimemuumiza sana na kudai kuwa akiiba mume wa mtu atakuwa anakosea pia!

Akizungumza na paparazi wetu, Shilole alisema kuwa adhabu aliyopewa ni kubwa mno kiasi ambacho  anashindwa kuelewa kwa kuwa sanaa ndiyo kazi inayompatia kula na hata kuwasomesha watoto wake hivyo kumfungia mwaka mzima ni kama kumtuma kutembea hata na waume za watu  ili maisha yake yazidi kusonga mbele.

“ Mimi naona sasa wananituma kuanza kusaka waume za watu kwa kweli kwa sababu mwaka mzima kweli na ni kazi ambayo naitegemea kwa kila kitu katika maisha yangu kwa nini  mtu usiwaze vitu vingine kama huna kazi ya kufanya jamani, yaani inaniuma sana,” alisema Shilole.