Kwa mwanamke ni jambo la faraja kupata mtoto baada ya kuolewa, lakini kupata mtoto kunaambatana na mabadiliko ya mwili kwa mwanamke. Ni wanawake wachche sana wanaobaki na miili yao mara baada ya kujifungua, lakini wengi wao hupoteza muonekano wa awali na kuongezeka mwili au tumbo na hivyo kupoteza muonekanao wake wa awali.
Jambo hilo kwa baadhi ya wanaume ambao mapenz kwa wenzi wao ni muonekanao wa nje wa mwanamke jambo hilo huzua kero na kupoteza hamu ya kukutana kimwili na mwenzi wake kama awali. hapo ndipo tatizo la kuchepuka linapoanza.
Ingawa pia tatizo la baadhi ya wanawake kuhamisha mapenz kwa watoto wao badala ya baba zao linasumbua ndoa nyingi, lakini hili la kupoteza muonekano na kuwa tipwatipwa limeonekana kuchangia wanaume wengi kupunguza mapenzi kwa wenzi wao.
Kwa ushauri tu, ni kwamba, wanawake wanapaswa kubadilika na kuanza kufanya mazoezi na kuzingatia mlo wao wa siku kwa kuacha kula hovyo hovyo ili kuepuka kupoteza muonekano wao wa awali. Si lazima kwenda kwenye nyumba za mazoezi kwa sababu kunahitaji gharama ambazo wengine si rahisi kuzimudu, lakini kwa mazoezi ya kutembea kwa umbali wa maili mbili kwa simu asubuhi au jioni kila siku na kufanya mazoezi ya kucheza mziki (Aerobics) kunaweza kusaidia kuweka mwili katika muonekano mzuri.
Ni ushauri tu.
Source: Mtambuzi