Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Afrika wakicheza
Ugenini huko Nchini Misri, Yanga wamefungwa 2-1 na Al Ahly na kuondolewa
katika michuano ya klabu bingwa Africa.
Mabingwa watetezi Tp Mazembe wakaondolewa katika michuano hiyo baada
ya sare ya 1-1 dhidi Wydad de Casablanca, na Casablanca wakisonga mbele
kwa ushindi 3-1.
Enyimba wakasonga mbele kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Etoile du
Sahel ,As Vita Club nao wakasonga mbele licha ya kufungwa kwa mabao 2-1
na Mamelod Sundowns .
Al Ahli Tripoli wakawachapa Asec Mimosas kwa mabao 2-1 lakini asec akisonga mbele kwa kwa jumla ya mabao 3-2
Kwa mujibu wa kanuni za CAF, timu zilizotolewa kwenye hatua ya 16
bora ya michuano ya mabingwa Afrika, zinakutana na timu washindi wa wa
hatua ya 16 bora kutoka kombe la sirikisho. Kwa maana hiyo, Yanga
inaangukia katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
;