Showing posts with label Ali Kiba. Show all posts
Showing posts with label Ali Kiba. Show all posts

Bifu la Diamond Platnumz na Ali Kiba Lazua Haya

Ni ukweli kuwa Diamond na Alikiba ni wasanii ambao hawapatani kwa muda mrefu.
Kutokana na ugomvi wao uliopo umepelekea mpaka mashabiki wao kuanzisha team, team hizi zinakuwa zinamsupport msanii wao na kumpinga mpinzani wao.

Diamond aliwahi kuhojiwa kwenye kipindi cha Sporah Show alisema, “Kuna wimbo wa Alikiba ‘Singel Boy’ nilimuomba Alikiba kuingiza sauti tulipokuwa studio alikataa na kusema kuwa nataka mteremko.”

Alikiba aliwahi kusema, “Kwenye wimbo wa ‘Lala Salama’ niliingiza sauti yangu lakini nilishangaa kuona sauti yangu imefutwa kwenye wimbo huo, kibaya zaidi ametumia melody yangu niliyorekodia mwanzo.”

Hakuna mwenye uhakika wa hili kuwa nani ni mkweli na nani anatudanganya. Ugomvi wao unazidi kuwa mkubwa kila siku, sasa hivi umeenda mbali zaidi mpaka msanii atakayekuwa karibu na mmoja kati ya hawa wawili wenye ugomvi mwingine anakuwa anachukia.

Ukiwa karibu na msanii mmoja unakosa support ya upande wa pili, hata kama umeingia kwenye mashindano hutaweza kupigiwa kura na mashabiki wa team nyingine. Hili linarudisha nyuma muziki wetu Angalia kilichotokea kwa Ommy Dimpoz hutataka kuangalia tena nyuma, unakumbuka Wema Sepetu mwanzo alikuwa team gani na sasa yuko wapi? Vipi Jokate kilichomtokea kwenye pande zote mbili kwa sasa unadhani atakuwa wapi tena?

Angalia support wanayopeana Wanigeria kwenye tuzo na muziki wao, hawaonyeshi tofauti zao japo wapo wengi hawapatani. Kwanini tugombee fito wakati tunajenga nyumba moja? Ni ukweli usihitaji ushahidi, Diamond akiingia kwenye tuzo zozote mashabiki wa Alikiba hawampigii kura wanaona ni bora kumpigia kura msanii wa nje ili Diamond akose hiyo tuzo.

Hilo pia lipo kwa upande wa pili kama Alikiba akiingia kwenye mashabiki wa Diamond hawampigii kura. Hata kama Wizkid ana ugomvi na Davido mashabiki wao hawawezi kumpigia kura Diamond au Alikiba ili ashinde tuzo.

Kuna haja wa kuweka tofauti pembeni na kuhakikisha muziki wetu unafika mbali zaidi, ‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, unajisikiaje tunaposhiriki kwenye tuzo za nje kwenye category moja unawaona wapo wasanii wanne kutoka Nigeria na mmoja tu ndiyo wa Tanzania.

Utajisikiaje siku ukiona Jay Z akapenda kufanya kazi na msanii wa Tanzania? Kwa hili lililopo sasa hivi kufika huko ni mbali sana, kila team inafanya msanii mwingine asifanikiwa. ‘Adui muombee njaa’, kwetu imekuwa tofauti tunaombeana wenyewe hiyo njaa.
Skendo:Kisa ujauzito wa Ali Kiba, Jokate aasi kanisani!

Skendo:Kisa ujauzito wa Ali Kiba, Jokate aasi kanisani!

IMG-20151118-WA0010Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo.
IMEVUJA! STAA wa muziki na mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amedaiwa kuasi kanisani kisa kikitajwa ni kutokana na ujauzito alionao, unaohusishwa na mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.
Chanzo makini cha gazeti hili ambacho kiko karibu na mwanadada huyo, kilisema kwa muda sasa amekuwa haonekani kanisani kama awali, na hata kwenye kwaya aliyokuwa akiimba ndani ya kanisa analosali la St. Peter lililopo Oystebay jijini Dar, haonekani.
“Yaani Jokate ujauzito alionao unamsumbua sana, ameacha hata na kuimba kwaya, kanisani haonekani kama ilivyokuwa zamani, pia hali hiyo inachangiwa na kwamba anaona aibu amebeba mimba nje ya ndoa, yaani hajaolewa ndiyo maana mara nyingi haendi kanisani,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo waandishi wetu walifunga safari mpaka kanisani kwa ajili ya kuonana na kiongozi wa kwaya aliyejulikana kwa jina moja la Catherine, ambapo walimkosa na kufanikiwa kuzungumza naye kwa njia ya simu baada ya kupewa namba zake.

“Jokate kwa sasa haimbi kwaya, amesitisha lakini sijui sababu ni nini,” alieleza kwa kifupi baada ya kuulizwa juu ya upatikanaji wa mrembo huyo maarufu kama Kidoti.
Ili kuleta mzani wa habari, Jokate ambaye ni mwandani wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba naye alitafutwa na kuelezwa habari hizo, ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Ni kweli siimbi kwaya mwaka sasa, ila kanisani sijaacha kwenda na siwezi kuacha kwenda na bado kazi za kanisa nyingine nafanya, sijaacha kwa sababu ya mimba bali ratiba zangu tu zilikuwa ngumu.”
Udaku:Mimba ya Jokate yazua balaa

Udaku:Mimba ya Jokate yazua balaa

JOKATE44
Jokate na Kiba wakipozi  kimahaba.
Kwani kimenuka? Siku chache baada ya kubumburuka kwa habari ya kunasa mimba ikimhusisha ‘mtoto mzuri’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mhusika mkuu akitajwa kuwa ni msanii nguli wa Bongo Fleva, Ali Kiba, ishu hiyo imezua balaa kufuatia familia ya mrembo huyo kushtushwa na hali hiyo, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
TWENDE OYSTERBAY

Mwishoni kwa wiki iliyopita, ‘kijumbe’ wa gazeti hili alitua getini nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar kwa lengo la kutaka kujua nini kinaendelea juu ya binti yao kunasa mimba nje ya ndoa ilihali familia hiyo inasifika kwa misingi bora na maadili ya kidini.

Gazeti hili lilipotia timu nyumbani hapo, lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wanafamilia hiyo aliyekuwa nje akifanya usafi ambaye bila simile ‘alifunua kinywa’ na kuweka hadharani mambo mazito.
GAZETI LA IJUMAA LAIBUA MAMBO

Kama anayeogopa jambo fulani, memba huyo wa familia ya Jokate alisema kuwa, mrembo huyo alikuwa akifanya siri kubwa juu ya ujauzito wake huo, lakini baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa, kuibua habari hiyo, familia hiyo, hususan mama yake mzazi (jina lipo), alizua utata mkubwa kwa binti huyo na kwamba alishtushwa na hali hiyo na kumlazimu kumkalisha ‘kitako’ Jokate ampe ukweli.

“Jokate alikuwa akifanya siri sana, lakini ninyi mlipoandika habari hiyo, hapakutosha, mama yake alimuitisha kikao na baadhi ya ndugu wengine, lakini Jokate hakutaka kuweka wazi juu ya hali hiyo.
sfud7zknmrs4955def775ef165
“Ninavyosikia, kuna uwezekano mkubwa wa Jokate kuhama hapa nyumbani akajitegemee ili kuififisha aibu hii kwani familia inadai amewatia aibu kwa kitendo chake cha kubeba mimba nje ya ndoa,” alidai mhusika huyo.

JOKATE ATOWEKA

Mnyetishaji wetu huyo aliendelea kudai kwamba, baada ya kuona anabanwa, alitoweka nyumbani hapo kwa siku mbili kabla ya kurejea na kuondoka kisha kurejea tena.

Kama kawaida ya gazeti hili kujiridhisha kwa kila habari kabla ya kuichapisha na kuwapelekea wasomaji wake, ‘kiranja mkuu’ wa dawati la Ijumaa Wikienda, mashine kubwa kwa habari za ndani za mastaa wa Kibongo, alimtafuta mrembo huyo kupitia simu ya mkononi na alipobaini kuwa mpigaji ni mwandishi wetu alishindwa kusema chochote zaidi ya kuiacha simu hewani na baadaye kuikata.
ATUMIWA SMS

Hata hivyo, ili kujizolea ushahidi madhubuti, mwanahabari wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) na kumsomea madai hayo, lakini hakujibu ujumbe huo licha ya simu ya mwandishi wetu kuonesha kuwa ujumbe ulikuwa umepokelewa (delivered).

KIBA KIMYAA

Pia, kwa upande wa Ali Kiba, simu yake ilionekana kutokuwa hewani muda mwingi, lakini mwandishi wetu alituma ujumbe wa kutaka kusikia chochote kutoka kwake ili akiiwasha simu akutane na ujumbe huo, lakini hadi gazeti hili linaenda kuchapishwa, hakuwa amejibu ujumbe huo achilia mbali kupiga simu hivyo jitihada zinaendelea.

Hata hivyo, mashabiki wa mastaa hao wameendelea kuwapongeza kwa namna ambavyo wamekuwa wakioneshana mahaba na kwamba suala la kupata mtoto ni jambo la heri bila kujali wamefunga ndoa au la.

GlobalPublisher

See How Female Fans Were Twerking And Dancing On Stage During Ali Kiba's Performance in Kenya

Koroga festival has emerged as the leading event in the country.

It gets to be attended by all the leading celebrities in the country and always sells out. Well, it does not lack in action either. A case in point is Ali Kiba's performance during last weekend edition.

On his final act, he called on some female fans on stage to dance with him and Oh Lord! they delivered. From the expats to the locals, especially one beautiful lady, they showed the Bongo star how it is done. Here are the videos;


Wakali Hawa Wakutana Kiulaini

Wakali Hawa Wakutana Kiulaini

Ali Kiba na Victoria Kimani. KWA kipindi cha hivi karibuni mastaa wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakichanua zaidi kimataifa kutokana na muziki huo kukua.Japokuwa wengi wao wameshafanya kolabo na mastaa mbalimbali wa Afrika hususan nchi za Kenya, Nigeria na Sauz lakini kuna mastaa wengine nchini bado hawajafanya na hata wengine kuwa na shauku ya kufanya kolabo na wasanii wa namna hiyo.

Ben Pol na Wangechi. Hivi karibuni, katika msimu wa tatu wa Coke Studio uliofanyika nchini Kenya, tumeshuhudia mastaa kama Ben Pol, Wangechi, Ali Kiba, Victoria Kimani, Vanessa Mdee na 2 face wakikutana kiulaiiiini na kutengeneza kolabo ambazo zitaanza kusikika Oktoba 10, mwaka huu. 


Vee Money na 2 Face (Nigeria) 
Vanessa Mdee ‘Vee Money’ anatarajiwa kutinga jukwaa moja na staa kutoka Nigeria, Innocent Ujah Idibia ‘2 Face’ na kukamua nyimbo zao zote kali. Ebu vuta picha 2 Face akiimbishwa Kiswahili ngoma za Vee Money kama vile Me & U na Come Over. 

Ben Pol na Wangechi (Kenya) 
Staa wa R&B Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ naye atakuwa ni miongoni mwa mastaa aliyekutana kiulaiiini na kufanya kolabo lake na staa kutoka Kenya, Wangechi. Mashabiki watarajie kumsikia Wangechi akiimba na Ben Pol ngoma kama Ningefanyaje, Jikubali pamoja na Sofia

Ali Kiba na Victoria Kimani (Nigeria)
Patakuwa hapatoshi pale, mkali wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ atakapopanda na staa wa muziki mwenye asili ya Kenya anayefanya shughuli za muziki nchini Nigeria, Victoria Kimani. Hebu vuta picha pale, Kimani anapokamu na Ali Kiba ngoma kama Chekecha Cheketua pamoja na Mwana.

Mahaba Niuwe!Ali Kiba na Jokate hakuna Siri tena...Angalia wakiwa Pamoja Uwanja wa Taifa!

Msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba akiwa na anayesemekana ni Mpenzi wake Jokate Mwegelo a.k.a Kidoti wakiwa wanaingia Uwanja wa Taifa kuutazama Mtanange wa Simba na Yanga hapo jana.Wawili hao siku nyingi walikuwa wakihisiwa ni wapenzi japokuwa Ali Kiba anakanusha habari hiyo ya kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na Kidoti.
Ni Sheeedah!Kweli hawa watu jamani hawana Uhusiano?Tazama Ali Kiba akiwa amemshika Jokate sehemu ya Naniii.
...Wakiwa wanapiga Story.

...Kuwa na Wivu ni Sunna jamani...Jokate akiwa anaiangalia kwa umakini simu ya Kiba.

Ali Kiba amtaja Mgombea Urais anayemtaka

Ni mwezi mmoja umebaki kufikia siku nyingine kubwa kwa Watanzania kupiga kura kumchagua Rais wanaemtaka, Wabunge pamoja na Madiwani kwenye Uchaguzi mkuu utakaofanyika October 25 2015.  
Tayari mpaka sasa tumeona Mastaa mbalimbali wa Tanzania ambao hawajaficha hisia zao ni nani wanamkubali zaidi kwenye kumpa uongozi wa nchi na nafasi nyingine zinazogombaniwa. 

Mwimbaji staa wa bongofleva Ali Kiba ameungana na mastaa wengine kama Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Steve Nyerere, Aunty Ezekiel, Ray ‘Vicent Kigosi’ na wengine kuiunga mkono CCM na mgombea wake Urais ambaye ni Dr. John Pombe Magufuli. 

Pamoja na kwamba Ali Kiba ameonekana kwenye headlines za kampeni za CCM, hakuwahi kuandika au kupost chochote kwenye kurasa zake kuhusu kiongozi gani anaeona ni sahihi kwake ila sasa ndio amefanya maamuzi hayo kwa mara ya kwanza.
A photo posted by Official Alikiba (@officialalikiba) on 
Diamond Platnumz na Ali Kiba Kumsindikiza Dkt. Magufuli Kwenye Ufunguzi wa Kampeni ya Urais

Diamond Platnumz na Ali Kiba Kumsindikiza Dkt. Magufuli Kwenye Ufunguzi wa Kampeni ya Urais


Staa wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’
KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa urais nchini, wasanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh Kiba ‘Aki Kiba’ kesho Jumapili wanatarajiwa kutumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Diamond na Ali Kiba ni sehemu ya wasanii wengi wa muziki na wale wa filamu watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Staa wa Bongo, Ali Kiba
Kitendo cha Ali Kiba na Diamond kupanda jukwaa moja ni nadra kutokea kutokana na upinzani uliopo kati yao, hiyo watu watakaofika kwenye uzinduzi huo watapata burudani ya bure ya aina yake.
Mbali na kutamba na nyimbo nzuri kwa kila mmoja wao, kumekuwa na upinzani mkali kuhusu msanii mkali wa kutawala jukwaa, hivyo wawili hao wanatarajiwa kutoa burudani ya kiwango cha juu ili kuendelea kuthibitisha ubora wao.
Magufuli amepata nafasi hiyo baada ya kupita katika mchujo wa watangaza nia zaidi ya 40 waliojitokeza ndani ya CCM. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Ni sheeedah!Jokate amtambulisha Ali Kiba apigwa chini kwao

Ni sheeedah!Jokate amtambulisha Ali Kiba apigwa chini kwao

jokate ali kiba
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kupigwa zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao kisha kukataliwa.
MINONG’ONO
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda harusi inayofuata itakuwa yao.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo haliwezekani huku sababu nne zikianikwa.
jokate
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
KIGEZO CHA DINI
Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho.
NDOA ZA MASTAA NI TATIZO?

Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.

KIGEZO CHA KABILA
Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka Jokate aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni Muha.
2alikiba-1
Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
KIGEZO CHA BONGO FLEVA

Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini.

KAMA DIAMOND
“Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate.

“Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho.

KIBA KAMA KAWA
Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha vikali akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo huyo.“Ulishawahi kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli bwana…hakuna kitu kama hicho,” alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa kuulizwa juu ya jambo hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa jamaa huyo ni mtu wake.

Chanzo: Globalpublisher