Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

Gerald Hando, Paul James waondoka Clouds FM

Gerald Hando na Paul James, wanadaiwa kuachana na Clouds FM, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
Wawili hao wamekuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha kituo hicho kwa miaka mingi.
Gazeti la Mwananchi limedai kuwa watangazaji hao wamemaliza mkataba na kituo hicho na hakijapenda kuwaongezea

Juma Nature adai mshindani wake kwenye muziki kwa sasa ni Diamond

 Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature amedai msanii pekee ambaye anaweza akashindana naye kwa sasa ni Diamond.
Akizungumza na tovuti ya Times Fm, Juma Nature ameomba wadau kuandaa tamasha ili washindanishwe.
“Watu wanamtukuza sawa lakini watuweke stage moja tuone nani atakamua, unajua tuseme ukweli bongo flava sasa mimi na Diamond ndio wapinzani pekee,” alisema Juma Nature.
Aliongeza, “Watu waandae pambano, na mpunga pia uwepo nioneshe na mimi nguvu yangu ilivyo mtaani,”
Nature amesema anaamini muziki wake aliyokuwa anafanya zamani una nguvu kubwa kuliko huu wa wasanii wa sasa.

Lady Jaydee atangaza mchongo huu kwa mashabiki wake

Lady Jaydee anataka kula dinner na mashabiki wake. Unachotakiwa kufanya ni kujirekodi na kupost video kwenye Instagram au Facebook ukiimba wimbo wake mpya, Ndindindi.
Lady Jaydee ameandika:
Katika watu wote waliotuma videos Wanaimba NdiNdiNdi Nawashukuru sana Wanaopenda kuendelea wanakaribishwa Ila nitakuwa nazi like huko huko Kwenye page zenu Kifuatacho sasa Nitachagua Clips 3 bora zilizokonga na kusuuza watu wengi Na watatu hao, nitafanya mchakato wa kula nao japo dinner Na ku hang nao siku yoyote nikiwa na event kubwa Majina nitataja baadae kidogo 1. 2. na 3.

Video MPYA: Kwenye video mpya za bongofleva ni hii mpya ya Amini ‘hawajui’

Kwa harakaharaka ni zaidi ya miezi kumi na mbili imepita toka mara ya mwisho nimetazama video mpya ambayo Amini yuko ndani, ni mwimbaji mwenye miaka yake kadhaa kwenye game ya bongofleva na sasa katuletea hii mpya, ukishamaliza kuitazama usisahau kumuandikia ajue watu wake wameipokeaje.

Picha za WEMA SEPETU akiwa katika Instagram Party Jijini Mwanza

 
Usiku wa tarehe 27, ulipambwa na Show ya Instagram Party kwa upande wa Mwanza 88.1, mastaa kadhaa wa Tanzania walikuwepo kunogesha Party kutoka Bongo movie Wema Sepetu, alikuwepo na kundi la Weusi liliwakilishwa na Joh Makini pamoja G nako.Party imefanyika Rock City Shopping mall Mwanza.
 
 
 

Jokate apata Shavu...Tyrese amtumia kupromote filamu yake mpya, lakini…

Tyrese ni miongoni mwa wamarekani weusi wenye ushawishi nchini humo – hasa kwa ubishi wake kwenye mitandao ya kijamii na jinsi anavyopromote kazi zake.
Hivyo kupewa shavu la walau picha yako kuwekwa kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye followers zaidi ya milioni 6.3, si kitu cha mzaha.
Picha ya mrembo wa Tanzania, Jokate Mwegelo imepata baraka zake (walau kwa muda tu) na kuwekwa kwenye ukurasa wa muigizaji huyo wa Fast and Furious wakati akipromote filamu yake fupi iitwayo ‘The Black Book.’
kiweka picha ya Jokate, Tyrese aliandika:
“I have movie studio looking at your comments!! #TheBlackBook has been unleashed… Go NOW!! Please? Click the link in my bio and watch the movie write your DETAILED comments below!!!!! #HappyEaster beautiful people around the world.”
Bahati mbaya aliifuta picha hiyo muda mfupi baada ya kuiweka