Showing posts with label Dkt. Slaa. Show all posts
Showing posts with label Dkt. Slaa. Show all posts

Mke wa DR SLAA Rose Kamili Ajitokeza Akiwa na Watoto wake na Kumchana Slaa na Kudai Ametumwa na CCM


Mbunge wa Viti  Maalumu kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana jioni kuhusiana na tuhuma alizozitoa mume wake kwamba waliishi kwa maisha ya kula mihogo na familia yake ili kuhakikisha chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo si la kweli walikuwa na maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa Dk.Slaa anapaswa awaombe radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo kuwa ni umaskini na kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli makubwa mihogo na viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.

akizungumzuia kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri mkuu mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita waziri mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea vizuri bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya waandishi wa habari kwamba hazungumzi na sumaye.
akizungumzia kuhusu kuja kwa lowassa chadema mama huyo alisema kuwa Dk.slaa alikuwepo katika kumkaribisha waziri mkuu mstaafu,Edward Lowassa kujiunga na chama hicho ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba hakushiriki na pia wakati chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake alisema kuwa viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na kumshawishi kutoludi kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa kuteuliwa na rais atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya awamu ya tano.

Kamili alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama tawala.
 Linus Slaa.
 Emiliana Slaa.
 Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.
 Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.

 Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo
Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose Kamili, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mume wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa chadema familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho jambo ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia) na Emiliana Slaa

BREAKING NEWS:Dr Slaa asema hakuwa Likizo ila aliachana na Siasa toka Julai

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), DK. Wilbroad Slaa amesema hakuwa likizo ila aliamua kuachana na siasa baada ya kutokubaliana na maamuzi ya chama chake yaliyotokea Julai 28,2015 saa 3 usiku.
-Asema lazima ajitokeze kusema na kuweka ukweli hadharani

-Asema sina tabia ya kuchengachenga nasimamia ninachokiamini
-Mengi yamesemwa na kuandikwa magazetini
-Sina ugomvi na kiongozi yoyote, maana siasa si ugomvi, sina chuki, sina hasira na mtu yeyote
-Siasa inayoongozwa na propaganda, ulaghai ni kuleta vurugu katika taifa na nimekataa hayo 
yote.

-Ni kweli nilishiriki katika majadiliano tangu mwanzo
-Misingi niliyoweka ni kwamba Lowassa atangaze kuwa ameachana na chama chake na aeleze anakwenda chama gani kwanza na ajisafishe na tuhuma zake
-Asema hawezi kumsafisha mtu bila yeye kufanya hivyo
-Asema alihoji kama Lowassa anakuja Chadema kama faida au mzigo (assets au liability)
-Asema anataka mgombea mwenye uwezo, sifa na kuiongoza Chadema kuiondoa CCM.
-Kama ni assets anakuja na akina nani? vijana wa mitaani, bodaboda au watu wa aina gani? ni viongozi makini?
-Asema aliambiwa kuwa anahama na wabunge 50, wenyeviti wa mikoa 22, wenyeviti wa CCM wilaya 82.
-Sikupewa majina ya wabunge wala wenyeviti.

-Nikatakiwa kuitisha kikao nikaitisha lakini sikuwa na majibu kama Lowassa ni 
Assets au Liability.

-Tangu 2004 sikuwahi kutofautina na mwenyekiti wangu bali tulitofautia kwa hilo.
- Asema aliandika barua ya kujiuzulu kwa M/kiti Prof. Safari barua ikachanwa.

-Siasa ni sayansi haitaki uongo wala ulaghai au propaganda

-Asema mke wake halipwi chochote kutoka Chadema na amekuwa akizunguka nchini kwa mshahara wa Dk. Slaa.

-Asema hakuwahi kupata vitisho kama alivyopata kipindi hiki, na Kumtaja Rostam Aziz kuwa ndiye mfadhili wa kampeni za Chadema.
Dkt. Slaa Kuibuka leo kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari

Dkt. Slaa Kuibuka leo kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari

Ni kweli katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amekua kimya toka Edward Lowassa ajiunge na CHADEMA akitokea CCM lakini August 31 2015 kituo cha TV cha STAR TV kimetangaza kuhusu Dr. Slaa kwamba atazungumza kwa mara ya kwanza leo September 1 2015.
Maneno ya mtangazaji msoma habari wa StarTV yanasema >>> ‘Dr Slaa amekua pembeni katika harakati za kisiasa lakini September 1 2015 atavunja ukimya huo kwa kuzungumza na vyombo vya habari Dar es salaam kuanzia saa saba mchana, mkutano huo utarushwa moja kwa moja mkutano huu