Showing posts with label Kajala. Show all posts
Showing posts with label Kajala. Show all posts

Kajala Is Pregnant..But This Man Who Isn't Quick Racka Is Named Behind Her Pregnancy


Actress Kajala Masanja is pregnant according to her instagram posts. she wants another child and she asked her followers to suggest the name of her unborn baby. Kajala and singer Quick Racka are said to be in love even Quick recently said they are together .
But word on the streets say the man behind her pregnancy is not Quick Racka but a high-profile leader and businessman. She is said to be five months pregnant, however Kajala is yet to say anything concerning rumors of the daddy of her unborn child.
Zaibuka Zengwe kwenye zile milioni 6 za Kajala kwa Tiffah

Zaibuka Zengwe kwenye zile milioni 6 za Kajala kwa Tiffah

IMG_0169.JPG
Imevuja! Yale mamilioni ya staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ aliyommwagia mwandani wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama zawadi ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princes Tiffah’ yamepigwa zengwe.
TIFFAH DIAMOND (4)
Awali, habari zilizolifikia gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko la Jumatano iliyopita zilieleza kwamba, Kajala alitumia takriban dakika ishirini kummwagia Zari ‘minoti’ ya elfu kumikumi kwenye pati ya arobaini ya Tiffah iliyofanyika nyumbani kwa Diamond, Madale-Tegeta jijini Dar, Jumapili iliyopita.

Katika maelezo yake kwenye habari hiyo, Kajala alisema kuwa alimtunza Zari kama waalikwa wengine walivyofanya bila kujali watu watasema nini.
Kwa mujibu wa Kajala, manoti hayo yalikuwa takriban shilingi milioni sita za madafu, jambo lililoibua maswali ikidaiwa kwamba, si kweli hakikuwa kiasi hicho na badala yake, mwigizaji huyo alitaka kujipaisha.
“Hata ukiangalia video za tukio hilo, utaona Zari alikuwa akicheza kitu kama Kibao-Kata wakati Kajala akichomoa ‘misimbazi’ kwenye waleti na kumtupia mama Tiffah.
“Ukweli ni kwamba hata waleti yenyewe ilikuwa nyembamba kiasi kwamba ingekuwa na kiasi hicho ingeonekana imevimba.
“Kilichotokea ni kwamba ile video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa inajirudiarudia na kuwafanya watu kuona kama Kajala alitoa noti nyingi kiasi hicho.
“Ukweli ni kwamba hata shilingi milioni mbili hazikufika. Si unajua tena Wabongo kwa kujipaisha? Habari ndiyo hiyo,” kilidai chanzo chetu na kuongeza:
Wakati mamilioni ya Kajala yakipigwa zengwe, kwa upande wake, mwigizaji mwingine wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson ambaye naye alidaiwa kumfanyia kufuru ya kummwagia Zari noti, naye ameibuka na kudai kwamba, yeye alitunza kiasi cha shilingi milioni tano ambazo nazo ziliibua maswali.
“Mimi nilimtumza Tiffah kama shilingi milioni tano hivi, kama kuna mtu mwenye swali atajijua mwenyewe kimpango wake,” alifunguka Aunt kwa kifupi.
KAJALA anapata Wapi Jeuri hii?

KAJALA anapata Wapi Jeuri hii?

Mjengo anaoishi mwigizaji Kajala Masanja.
FEDHA inaongea! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji Kajala Masanja kupanga kwenye mjengo mpya wa maana na kuushehenesha samani na ‘vikorombwezo’ kibao hadi kufikia hatua ya watu kuhoji, amepata wapi jeuri hiyo ya fedha? Ijumaa limenasa mchapo kamili.
Kajala ambaye awali alikuwa akiishi maeneo ya Sinza-Madukani, kwa sasa amehamia katika mjengo huo mpya uliopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo, ndani ya mjengo huo, Kajala anaishi na mwanaye Paula huku akiwa amewaajiri wafanyakazi wa ndani watatu na kulindwa na kampuni maalum ya ulinzi.
“Yani Kajala ananuka hela. Mjengo wake mpya una kila kitu ndani. Ukiingia unaweza kupagawa kutokana na vitu vilivyomo ndani. Watu tunajiuliza ni nani anayempa jeuri hii maana filamu pekee haziwezi kufanya matusi haya,” kilisema chanzo hicho.
...Sebuleni.
Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alitia timu nyumbani hapo kwa Kajala na kujionea nyumba hiyo ya kifahari aliyopanga sambamba na ‘mazagazaga’ kibao ya thamani yaliyomo ndani.
Alipoulizwa amepata wapi jeuri ya kupanga nyumba hiyo ya gharama ambayo hakutaka kutaja bei ya kodi, kuajiri wafanyakazi watatu na kampuni ya ulinzi, Kajala alidai mambo yote hayo ameyafanikisha kwa kazi ya mikono yake na si vinginevyo.



“Unajua kuna kipindi cha nyuma nilitengeneza filamu zangu kama tano na nilikuwa na maana hata kama nisingepata zile hela kwa wakati ule lakini nilijua baadaye nitapata hela nzuri na nitatengeneza maisha yangu hivyo sasa ndiyo nimevuna matunda ya sinema hizo na kufanya haya unayoyaona,” alisema Kajala licha ya nyuma ya pazia kuwepo na madai kuwa kuna kigogo anamuweka mjini.

Chanzo: Global Publishers

Kajala aamua kufungukia kuhusu kuingia kwenye siasa za kibongo

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi kugombea.

Akizungumza juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama hicho.

“Mimi siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona wenzanguwote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza kuchukua,” alisema Kajala.