Showing posts with label Riyama Ally. Show all posts
Showing posts with label Riyama Ally. Show all posts

Hatimaye! Riyama Ally amelipiwa Mahari na Mpenzi wake 'Sharobaro'

 
Hatimaye! Taarifa ikufikie kwamba, staa wa kitambo wa Bongo Muvi, Riyama Ally amelipiwa mahari na mpenzi wake ‘sharobaro’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Haji  Mwalimu ‘Leo Mysterio’ huku mipango kabambe ya ndoa ikiendelea.
Riyama ameliambia Wikienda kuwa, anamshukuru Mungu kumpata mtu anayeona ndiye anamfaa katika maisha yake na tayari sasa ni mchumba rasmi wa mtu, tena kijana anayempenda kwa dhati.
“Sasa hapa ndiyo nimefika kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye mapenzi ya kweli kwangu. Pia nafsi zetu zimeendana, hapa namuomba Mungu anyooshe mambo yaende kama vile tulivyopanga,” alisema Riyama ambaye amekuwa ‘singo’ kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Mysterio alisema kuwa anaamini safari yake ya muda mrefu imefika kwa kuwa amempata mwanamke anayempenda kutoka ndani ya uvungu wa moyo wake na kwa upande wake taratibu zote za uchumba amemaliza, anasubiri ndoa watakayofunga hivi karibuni.

Mchumba wa Riyama Ally Afunguka 'Ukipata Mtu kama Riyama Usichelewe Kumuoa'


Leo Mysterio amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwa sasa tayari yeye amefanya maamuzi ya kuishi na Riyama na muda wowote kuanzia sasa wanaweza kufunga ndoa kwani hatua za awali tayari wameanza kuzifanya.

"Unajua Riyana ni mtu ambaye ana huruma sana, ana akili pia ana mapenzi ya kweli kwangu na amekuwa akinisaidia katika kazi zangu hivyo nimefikia wakati nimeona ni bora nimuweke ndani kwani nimeridhika na yeye kwa kila kitu, ndiyo maana sijataka kuchelewesha kwa sababu yeye ndiye mwenye sifa kwangu" Alisema Leo Mysterio

Mbali na hilo Leo Mystereo amesema hajakurupuka katika maamuzi sababu yeye tayari alishafahamiana na Riyama Ally kwa zaidi ya miaka kumi uliyopita, lakini pia hajawahi kumuweka wazi mpenzi wake yeyote yule kipindi cha nyuma lakini mpaka amefikia hatua hii amejiridhisha na kuona kuwa Riwaya ndiye chaguo lake la kweli.