Showing posts with label Bongo Movies. Show all posts
Showing posts with label Bongo Movies. Show all posts

Baada ya Talaka… Wastara Sasa Hali Mbaya!

Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma.
 Anahitaji maombi! Baada ya kupewa talaka kufuatia madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis Juma kisha kuzimia na kulazwa hospitalini kwa mshtuko, hali ya kiafya ya staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma sasa inadaiwa kuzidi kuwa mbaya.
Juzi kati(Alhamisi), Risasi Jumamosi lilimtembelea Wastara kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Herry Heath Centre mkoani hapa na kumkuta akiwa hajitambui huku wauguzi wakithibitisha hali yake kuwa si nzuri, wakiendelea kupigania uhai wake.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuzungumza na Wastara lakini ilishindikana kutokana na hali yake kuwa mbaya kiasi cha kushindwa kuzungumza.

Akielezea hali ya Wastara, babu wa staa huyo aliyekutwa hospitalini hapo, Abdulaziz Babu ambaye naye ni msanii maarufu wa filamu mkoani hapa alikuwa na haya ya kusema:
“Tangu aolewe na huyo Sadifa, ndoa yake imekuwa na migogoro mingi. Majuzi Wastara aliamua kuachana na mheshimiwa huyo kisha akabeba vitu vyake na kuja kwangu hapa Morogoro.
“Aliamua kuja kwangu kupumzisha akili yake. Chanzo cha mjukuu wangu kuugua ni huyo mheshimiwa aliyekuwa anaposti kashfa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya mjukuu wangu.
“Baada ya kuona hizo kashfa ndipo mjukuu wangu akapatwa na presha na kisukari kisha akapoteza fahamu.

“Niliamua kumkimbiza hapa hospitalini na hali yake ni mbaya kama unavyomuona. Kikweli hali hii inasikitisha na inaniumiza sana lakini najua Mungu anampigania.”
Alipoulizwa kama Wastara akipona na kuweka mambo sawa na Sadifa atarudi kwenye ndoa yake, babu huyo alijibu kwa jazba:
“Hatuko tayari mtoto wetu kuendelea kupata manyanyaso kama aliyokutananayo kwa kipindi kifupi kutoka kwa huyo mwanaume.
“Kwanza Wastara mwenyewe anajuta na ameapa kutorudi tena kwa Sadifa.”
Katika hali nyingine, wauguzi walijikuta wakiacha majukumu yao na kurundikana kwenye wodi hiyo kumshuhudia Wastara huku mashabiki wake wakizuiwa nje kwani walifurika hospitalini hapo kutaka kumjulia hali lakini walikataliwa kufuatia hali mbaya aliyokuwanayo msanii huyo.

Kuhusiana na tuhuma za kumnyanyasa Wastara na juu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo, kwa upande wake Sadifa aliliambia gazeti ndugu la hili, Ijumaa kuwa yeye siyo mgonjwa wa akili.
Alisema: “Wastara ni mlemavu, hana baba wala mama halafu leo hii aniseme vibaya?”
Alisema kuwa hadi akaamua kumuoa ni kwamba alimpenda hivyo anashangaa kwa nini amseme hivyo.
Wastara amepitia katika uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa. Awali alizaa na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Msafiri Kombo ‘Solo Thang’.

Mwaka 2000, alifunga ndoa na Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares. Baadaye alifunga ndoa na msanii mwenzake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye kwa sasa ni marehemu na alizaa naye mtoto mmoja aitwaye Farheem kabla ya kufunga ndoa na Sadifa alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Bond Bin Suleiman.

Mchumba wa Riyama Ally Afunguka 'Ukipata Mtu kama Riyama Usichelewe Kumuoa'


Leo Mysterio amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwa sasa tayari yeye amefanya maamuzi ya kuishi na Riyama na muda wowote kuanzia sasa wanaweza kufunga ndoa kwani hatua za awali tayari wameanza kuzifanya.

"Unajua Riyana ni mtu ambaye ana huruma sana, ana akili pia ana mapenzi ya kweli kwangu na amekuwa akinisaidia katika kazi zangu hivyo nimefikia wakati nimeona ni bora nimuweke ndani kwani nimeridhika na yeye kwa kila kitu, ndiyo maana sijataka kuchelewesha kwa sababu yeye ndiye mwenye sifa kwangu" Alisema Leo Mysterio

Mbali na hilo Leo Mystereo amesema hajakurupuka katika maamuzi sababu yeye tayari alishafahamiana na Riyama Ally kwa zaidi ya miaka kumi uliyopita, lakini pia hajawahi kumuweka wazi mpenzi wake yeyote yule kipindi cha nyuma lakini mpaka amefikia hatua hii amejiridhisha na kuona kuwa Riwaya ndiye chaguo lake la kweli.
Msanii alewa ashindwa kutembea

Msanii alewa ashindwa kutembea

MSANII ALEWA (1)
Msanii wa filamu za Bongo, Glasnost Kalinga akilia wakati marafiki zake wakitaharuki.

MSANII wa filamu aliyefahamika kwa jina la Glasnost Kalinga hivi karibuni alipata aibu ya aina yake baada ya kulewa na kushindwa kutembea.
Msanii huyo alinaswa na kamera yetu maeneo ya Afrikasana, Sinza saa 6 usiku ambapo alionekana akiwa amelala chini huku marafiki zake wakijaribu kumkokota bila mafanikio.
MSANII ALEWA (5)…Akigalagala
Akizungumnza na Ijumaa katika eneo la tukio, mmoja wa marafiki wa msanii huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alidai kuwa, hakuna chochote kibaya kilichompata ila alizidiwa na pombe.
MSANII ALEWA (4)…Wote wakishangaana
“Hana tatizo, ni pombe tu ndiyo maana yuko katika hali hii. Tulitoka vizuri viwanja tukiwa ndani ya Bajaj lakini tulipofika hapa na kushuka tukashangaa mwenzetu kasinzia, tulipomuamsha akaonekana hajitambui, aliposhuka ndiyo kashindwa kutembea,” alisema shosti huyo.
MSANII ALEWA (3)Hali ya sintofahamu ikiendelea
Baada ya paparazi wetu kunasa tukio hilo usiku, kesho yake asubuni alimpigia simu Glasnost na kumuuliza ilikuwaje ambapo alisema kwa kifupi kuwa hajui kilichotokea kwani ndiyo alitoka kuamka.
MSANII ALEWA (2)…Wakiondoka eneo hilo
“Ndiyo nimeamka hapa, ila kwa kweli sijui hata kilichotokea jana ,” alisema msanii huyo ambaye ameonekana kwenye filamu mbalimbali kama vile Bikira, Mwadawa na nyinginezo.

Chanzo: Global Publishers
Nora adaiwa kunasa mimba!

Nora adaiwa kunasa mimba!

NORA


MSANII wa kitambo katika tasnia ya maigizo na filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ anadaiwa yuko ‘kitumbo ndii’ na ndiyo sababu ya kukaa kimya tena kwa siku za hivi karibuni, Ijumaa linadokeza.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar mmoja wa rafiki wa muda mrefu wa Nora ambaye pia ni msanii wa muda mrefu (jina tunalo), alisema kwa sasa Nora anatumia muda mwingi kuwa ndani kutokana na kile alichokiita “kupelekwa mputa” na mimba hiyo aliyodai kuwa changa bila kutaja umri wake.
Baada ya kupata habari hizo Ijumaa lilimtafuta Nora kupitia simu yake ya mkononi, ambapo baada ya kusomewa madai hayo alisema:
“Sasa kama ni kweli kuna ajabu gani juu ya hilo? Kwani mimi ni mwanaume? Mbona unaingilia sana mambo yangu binafsi, achana na mimi bwana,” alisema Nora na kukata simu kabla ya kuizima.

Rose Ndauka: Nipo Tayari Kuolewa Na Yeyote!


ROSE Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke aliyekamilika na mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari kuolewa na kuishi kama mama na mwanaume yeyote.


Akichonga  Rose alisema japo mume bora anatoka kwa Mungu na kwamba anangojea aliye chaguo lake, lakini amechoshwa na hali ya kuishi bila ndoa.

“Mimi kama mwanamke ninayetoka kwenye familia yenye maadili, inafika wakati natamani kuishi katika ndoa, natamani kuwa na familia yangu na mume wangu na kwa sasa akitokea yeyote, nikajihakikisha kuwa anavyo vigezo ninavyovihitaji, hakika niko tayari kuanzisha naye safari ya maisha,” alisema Rose.

Awali Rose alikuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ‘King Chiwaman’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mwishoni mwa mwaka jana waliachana.
Aunt Ezekiel atoa ya Moyoni kuhusiana na LOWASSA

Aunt Ezekiel atoa ya Moyoni kuhusiana na LOWASSA

aunt Ezekiel qqqqqqqqqqqqqqq
Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wasanii kwenye tasnia ya Bongo Movies wao walishatangaza hivi karibuni kuwa imani yao katika uchaguzi mwaka 2015 wanaamini CCM kitashinda kupitia mgombe wake Dk. John Pombe Magufuli.

Agosti 4, 2015 kupitia kwenye mtandao wa instagram mwigizaji Aunt Ezekiel ameamua kuyatoa ya moyoni na kumtaja mgombea wa urais  ambaye anaimani naye kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuyaandika haya >>> ‘Tunaimani na Lowassa..Mungu bariki Tanzania, Mungu bariki Africa