Kila Mtu Maishani kwake anaye mpenzi wake wa kwanza. Kuna walio na bahati ya kuwa na wapnz wao wa mwanzo mpaka leo na wengine wapo katika ndoa zao. Mungu awape kila la kheri. Ila tupo wa kina sisi, tulishapendaga saana zamani, kwa bahati mbaya hatukurudishiwa upendo wa kiwango sawa na hao tuliowapenda kwa moyo woote, na leo tupo katika mahusiano mengine. Kuna uwezekano miongoni mwetu tumeshawasahau hao tulio wapenda kwani Mungu ameshatupa mahusiano mengine ambayo ni bora na matamu zaidi kiasi kwamba hatuna hata hamu ya kuyafikiria ya nyuma. Ila pia tupo katika sisi, japokuwa tupo katika mahusiano mengine, lakini kila siku tunawakumbuka wenza wetu wa awali, tunajutia katika nafsi zetu kwanini hatupo nao, na kama tutapewa nafasi ya kuomba kitu kwa Mungu na kukubaliwa basi leo hii tungeomba kuwa pamoja na wenza wetu, Wapnz wetu wa Mara ya Kwanza.
Haimaanishi Mpnz wa kwanza awe ni yule aliyemtoa Bikira Mwanamke au aliyekuwa wa kwanza kufanya mapnz na mwanamke, hapana, hapa namzungumzia Mpnz yule ambaye aliuteka moyo wako wote, roho, akili na nafsi, yeye ndo akawa kila kitu kwako, bora usile yeye ale, yule aliyekufanya Chozi likakutoka kwa ajili yake, yule ambaye ukianza kuelezea ni jinsi gani una hisia kwake basi utamaliza vitabu na wino na bado ukawa na la kuandika........
Kuna Kisa kimetokea maeneo fulani ambapo wamefumaniwa watu wazima wakifanya mapnz katika nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake. Walipokamatwa na raia wema katika utetezi wao nimepata jambo la kutahadharisha. Jamaa alisema kwamba "Huyu mwanamke mimi ndio mwanaume wake wa kwanza, nnampenda ingawa kwa sasa ameolewa, ni muda mrefu hatujaonana, leo kama bahati nimekutana nae maeneo haya halafu sina hela ya kwenda "Guest" ndo maana tumeona tuje hapa tujienzi"

;