Waziri Mkuu Mstaafu, Ndugu Frederick Sumaye hatimaye leo ametangaza Rasmi kukihama chama chake cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Umoja wa Katiba ya Wannanchi (UKAWA) japokuwa Sumaye hakuweka wazi ni Chama gani ataingia.
Sumaye ameitoa Kauli yake Leo kwenye Hoteli ya Ledger Plaza,Kunduchi jijini Dar Es Salaam katika Mkutano na Waandishi wa Habari ulioandaliwa na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Mbali na kutangaza kukihama CCM, Mheshimiwa SUMAYE alielezea Mapungufu kibao ya CCM katika Mchakato wa kumtafuta Mgombea wa Urais kupitia CCM.
Pia Ndugu Sumaye alikosoa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulhaman Kinana nchi nzima kwa kuikosoa Serikali wakati ndiyo Chama kilichoiunda Serikali. Sumaye alisema,
"Ziara ya Katibu Mkuu ilikuwa ni kuipaka Matope Serikali na si kukijenga chama".
Ndugu Sumaye pia alieleza kuwa CCM imepoteza uelekeo na kusema kuwa hata chama kifanye jambo lipi lakini ifikie hatua lazima watu watakichoka.
Na amehaidi kumsaidia Lowassa kufanikisha Malengo aliyoyataka kuyafanya kama angeteuliwa kuwa Mgombea wa Urais kupitia CCM.
;