Photos:Kylie Jenner steps out in skintight suede mini-dress

Kylie Jenner looked stylish in a skintight suede mini-dress as she met with boyfriend Tyga for lunch yesterday. More photos...









Michezo:Nyoso afungiwa miaka miwili

Michezo:Nyoso afungiwa miaka miwili

Katibu mkuu wa TFF, Mwesiga Selestine
Katibu mkuu wa TFF, Mwesiga Selestine
Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Juma Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya John Bocco msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania bara
Juma Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya John Bocco msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania bara
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa  lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
  1. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
  2. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
  3. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
  4. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo
Zari atumika kumdhalilisha Wema...Kisa kuzaa na Diamond Platnumz!

Zari atumika kumdhalilisha Wema...Kisa kuzaa na Diamond Platnumz!

zarinah
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’

WATU wabaya! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia watu wanaoasadikiwa kuwa ni wafuasi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutumia jina na picha ya mwandani wa sasa wa staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumdhalilisha mpenzi wa zamani wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tangu Zari, ambaye ni mjasiriamali maarufu aliyemzalia Diamond, amfanyie mwanaye Latiffah ‘Tiffah’ sherehe ya kumtoa nje kwa mara ya kwanza (Arobaini).
ZARI (1)
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
KIINI CHA UDHALILISHAJI
‘Kirusi’ wa kwanza kuanzisha udhalilishaji huo alijitambulisha katika mtandao wa Instagram kwa jina la Who is Boss ambapo aliweka picha inayomuonyesha Zari akiwa amembeba mtoto wake na Wema akiwa amembeba mbwa kisha kusindikiza ujumbe uliosomeka:
“Ukibeba mimba utalea mtoto na ukitoa mimba utalea mbwa.”
TIMU DIAMOND ZAMSHAMBULIA WEMA
Mara baada ya Who is Boss kuweka picha na ujumbe huo, wafuasi wa Diamond (Team Diamond) walianza kumshambilia Wema kwa kumkejeli na kumtukana matusi mazito yasiyoandikika gazetini.
Wafuasi hao walimtuhumu Wema kuwa alichezea ujana kwa kutoa mimba matokeo yake kwa sasa analea mbwa wakati mwenzake Zari ametumia ujana wake vizuri na ndiyo maana amemzalia Diamond.
wema (3)
Wema Sepetu ‘Madam’.
WEMA ABUBUJIKWA MACHOZI
Chanzo kilicho karibu na Wema kilipenyeza habari kuwa alipopewa taarifa hizo za kudhalilishwa mtandaoni, alisikitishwa na kejeli hizo kiasi cha kumwaga machozi kwani suala la kutopata mimba yeye linamtesa hivyo mtu anapomkejeli, anaumia sana.
“Huwezi amini Wema amemwaga machozi. Anaumizwa sana na hawa watu wanaomkejeli kila kukicha mitandaoni hususan katika suala linalohusu mtoto,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambaye alikiri kukejeliwa na kusema ameumizwa na taarifa hizo hivyo analiomba jeshi la polisi nchini kuwashughulikia watu hao kupitia sheria mpya ya mtandao.
“Sijam-follow huyo mtu, ninapewa taarifa na watu, naamini atapatikana tu tena siku si nyingi maana watu wanapenda kutukana wenzao bila sababu za msingi,” alisema Wema.
MAMA WEMA ACHARUKA
Mbali na Wema, udhalilishaji huo ulimtibua mama mzazi wa staa huyo, Miriam Sepetu ambaye alisema hawezi kuacha suala hilo lipite hivihivi, atahakikisha ‘anadili’ na watu wote wanaomuandama mwanaye mitandaoni na kwa kuanzia watamshtaki Who is Boss.
“Hata siku moja sio haki kwa kweli, huwezi mtu ukasema kuwa analea mbwa na wakati hakuna hata mtu mmoja aliyempima mtoto wangu  na kujua hawezi kuzaa mtoto kwa hili sitokaa kimya nitamshtaki na piga ua, atapatikana tu,” alisema mama Wema.
AZIDI KUTIRIRIKA
Mama huyo alienda mbele zaidi na kusema kumekuwa na vitu vingi ambavyo vimekuwa vikimdhalilisha mwanaye na kumletea picha mbaya katika jamii, hivyo mamlaka zinazohusika na mitandao zinabidi zichukue hatua stahiki.
“Kwa hili sitanyamaza na itakuwa mfano maana watu wamezidi kudhalilisha   wenzao, TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) lazima ianze kufanya kazi yake na iwe fundisho,” aliweka nukta Mama Wema.

Chanzo: GPL


Udaku:Bela atafuta kiki kwa picha za utupu

Udaku:Bela atafuta kiki kwa picha za utupu

ISABELA.png
KATIKA kile kinachoaminika kama ni kutafuta kiki, Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda amepiga picha za utupu na kuzitupia katika mitandao ya kijamii akiwa katika pozi mbalimbali.

Rafiki yake mmoja (jina linahifadhiwa) aliyelinyetishia gazeti hili kuhusu uwepo wa picha hizo, alisema kwa jinsi picha hizo zilivyo ni wazi kuwa endapo sheria ya mtandao itafanya kazi yake, basi mrembo huyo atakuwa matatani.
Gazeti hili lilipowasiliana na Isabela baada ya kuziona picha hizo na kutaka kujua jinsi atakavyoshughulika na sheria ya makosa ya mtandao alisema; “Picha siyo kitu cha kunifanya nishtakiwe kwa sababu simtukani mtu, wala mavazi yangu siyo sababu ya kuchukuliwa hatua labda wanaopitia sheria hii wawe hawana kazi ya kufanya.

Mademu Maarufu wazuri wanaokimbiza Afrika Mashariki


Irene Uwoya Wa Bongo Movies
Linah Bongo flava singer
Cindy musician from Uganda
Queen Darleen Bongo flava singer (Diamond Young sister)
Wolper Bongo movies. 
Shilole Actress Bongo movie and Bongo Flava singer 

Photos:Kim Kardashian's heel buckles under her weight

The heel of the sandals of the heavily pregnant star buckled under her weight as she ran errands in LA yesterday.
JAY-Z Vs DIAMOND, TIFFAH Vs BLUE IVY, WANAVYOFUNIKA KWA REKODI

JAY-Z Vs DIAMOND, TIFFAH Vs BLUE IVY, WANAVYOFUNIKA KWA REKODI

Jay Z na Beyonce...Wakiwa na mtoto wao Blue IvyDiamond Platnumz na mpenzi wake Zarinah  Hassan 'Zari the Boss Lady' wakiwa na mtoto wao, Latiffah Nasbul 'Tiffah'.
Mastaa na shoo za ‘kiprofesheno’ SEAN Carter ‘Jay-Z’ ni jina kubwa sana duniani kufuatia mchango wa msanii huyo katika gemu la muziki wa Hip Hop. Kupitia umaarufu wa jina lake, umeweza kumpatia mafanikio makubwa na hata kumsaidia mwanaye, Blue Ivy Carter kuvunja rekodi akiwa bado tumboni kwa mamaye siku chache tu baada ya kuzaliwa.
Jambo hilo lililotokea kwa Jay-Z ndilo limetokea pia kwa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na mwanaye Tiffah. Katika makala haya yanachambua baadhi ya vitu vinavyoshabiiana kati ya mastaa hao;
Jay-Z na Blue Ivy Historia ya msanii huyu imekuwa ikiwavutia wengi kutokana na jinsi alivyoanza kazi yake ya muziki akiuza CD mkononi kutokana na kukosa msimamizi mpaka mwaka 1996 alipoachia albamu yake ya kwanza iitwayo Reasonable Dought iliyofanya vizuri.
Kwa upande wa ujasiriamali na uwekezaji, anamiliki Klabu 40/40, ni mhisani katika kampuni ya nguo za Rocawear, mdau katika Studio ya Roc- A-Fella na mmiliki wa Kampuni ya Roc Nation.
Kwa upande wa mwanaye, Blue Ivy aliyemzaa na mwanamuziki wa R&B, Beyonce Knowles alianza kuvunja rekodi kabla hata hajazaliwa baada ya mamaye kutangaza kuwa ana ujauzito kwenye Tamasha la Ugawaji Tuzo za MTV mwaka 2011 ambapo ndani ya sekunde moja zaidi ya watu 8,868 walishare taarifa hiyo.
Blue Ivy alivunja rekodi nyingine baada ya kuzaliwa kwa kutajwa kuwa mwanamuziki mdogo kuwahi kutokea kwenye Chati za Billboard kwa kushirikishwa kwenye wimbo wa baba yake uitwao Glory. Mbali na rekodi hizo mtoto huyo mwenye miaka mitatu kwa sasa amepata dili kwenye makampuni mengi ya mavazi, ameshirikishwa kwenye nyimbo kadhaa za wazazi wake na inasemekana ndiye motto maarufu zaidi duniani. Diamond Platnumz na Tiffah Diamond pia ana historia ya kuvutia ambapo mwaka 2009 alitoa Wimbo wa Nenda Kamwambie kasha mwaka 2010 kuvunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuchukua tuzo tatu za Kili Music.
Diamond amewahi pia kuvunja rekodi kwa kuwa msanii wa kwanza kuuza zaidi ya kopi 1200,000 za albamu na msanii wa kwanza kufanya shoo iliyoitwa Diamond are Forever na kuuza zaidi ya tiketi 1,500 kwa kiingilio cha Sh. 50,000.
Mbali na tuzo nyingi alizochukua, Diamond amewahi kuwa balozi wa makampuni mengi nchini ikiwemo Coca Cola.
Kwa upande wa bintiye Tiffah, mbali na kupata umaarufu tu akiwa tumboni mwa mama yake Zarinah Hassan, alianza kuvunja rekodi ya kwanza kwa kupata zaidi ya
wafuasi 2,000 kwenye ukurasa wake wa Instagram chini ya saa 24 tangu kuzaliwa kwake. Lakini pia hadi anafanya sherehe ya kutimiza siku 40, tayari kwenye ukurasa huo alikuwa na wafuasi 126,000 ambao umemfanya kuwazidi baadhi ya mastaa nchini.



Mbali na kuvunja rekodi hizo ambazo hazijawahi kuwekwa na mtoto yeyote yule wa staa Bongo,Tiffah pia ni balozi wa Pugu Mall na Msasani City Mall kwa upande wa maduka ya nguo za watoto ambapo anavishwa bure kwa mwaka mzima.

keeping Up with Princess Tiffah

 At less than three months old,Princess Tiffah's life is super interesting already...Her parents Zari and Naseeb "Diamond Platinumz add a bit into the fun
 Zari looking stunning already as she reenters the world after her delivery
 How stylish and fab is this?

The Princess living her royal life,indeed...Can't imagine her first birthday bash!

Kitaifa:Lowassa avunja mkutano Tanga

Baadhi ya wananchi wakiwa wamepoteza fahamu kutokana na msongamano kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa uliofanyika kwenye Uwanja wa Tangamano mkoani Tanga jana. 


Tanga. Mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa jana alilazimika kukatisha mkutano wake wa kampeni kabla ya muda, kwa kuhofia usalama wa wananchi waliofurika kuzidi uwezo wa Uwanja wa Tangamano mjini hapa.

Lowassa aliwasili jijini Tanga saa 10.20 jioni kwa helkopta ambayo wakati ikiwa angani ikitafuta nafasi ya kutua uwanjani hapo, Tambwe Hizza aliwaeleza wananchi kwamba kutokana na watu kuwa wengi kwenye uwanja huo, hakukuwa na mahala pa kutua, hivyo inaenda kutua uwanja wa ndege.

Msafara wa Lowassa aliyekuwa katika gari aina ya Landcruiser ya rangi nyeusi ulitokea uwanja wa ndege kwa kuongozwa na magari ya polisi, lakini hata hivyo hakuweza kufika mapema Tangamano kwa sababu watu walikusanyika kwa wingi kwenye barabara alizopita kumshangilia.

Alipofika Tangamano watu waliokuwapo uwanjani hapo kwa maelfu walianza kuminyana wakigombea kumuona huku wakimshangilia, “rais, rais, rais”.

Mara baada ya kuwasili katika jukwaa alilokuwa amepangiwa kukaa, watu walipiga kelele wakitaka apande jukwaani ili wamuone, kitendo kilichomlazimisha meneja wa kampeni wa mgombea huyo, John Mrema kumuomba awasalimie kabla ya kuketi.

Kitendo cha Lowassa kusimama na kupanda jukwaani, kilisababisha uwanja kuripuka kwa mayowe kumshangilia huku wakiimba rais, rais, rais hata alipokwenda kukaa wananchi waliendelea kuimba.

Wakati Lowassa akisalimia, msongamano wa watu uliongezeka na hivyo kusababisha wanawake kuanguka kwa kukosa pumzi jambo, lililomlazimu Mrema kuwaita wahudumu wa msalaba mwekundu kutoa msaada.

Zaidi ya watu 50 walianguka na kubebwa na polisi pamoja na wahudumu wa Msalaba Mwekundu na kupelekwa sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia.

Ofisa wa shirika la Msalaba Mwekundu alikaririwa akisema idadi ya watu waliozimia katika mkutano huo ilikuwa kubwa ambayo haijawahi kutoka katika mkutano mwingine mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwambeji alisema baadaye kuwa amepata faraja kwa kuwa watu wote waliokuwa wamezimia walizinduka na kurudi nyumbani salama na hakukuwa na majeruhi.

Hata hivyo baada ya mkutano huo, polisi walilazimika kupiga mabomu mawili ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wanarudi nyumbani kwa maandamano katika barabara ya Ngamiani. Akizungumzia tukio hilo RPC Mwambeji alisema walikuwa wanazuia barabara na kusababisha msongamano.

Sumaye aamua kumaliza mkutano

Wakati hali hiyo ikiendelea, Meneja wa kampeni alimkaribisha Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na alipopewa kipaza sauti alitumia dakika saba kuwatuliza wananchi waliokuwa wakisukumana kugombea kumuona Lowassa.

Sumaye aliwashukuru wakazi wa Tanga kwa kujitokeza kwa wingi na kubainisha kwamba CCM haina pa kutokea.

“CCM inatangaza kwamba Tanga ni ngome yake, hii inaashiria kwamba safari hii wana-Tanga wanahitaji mabadiliko kwa sababu umati huu mkubwa ambao sijawahi kuuona, umekuja kumshuhudia rais wa awamu ya tano,” alisema Sumaye.

Hata hivyo, Sumaye hakumaliza hotuba yake baada ya kuona watu wanaoanguka kwa kukosa hewa ikiongezeka, ndipo akasema anamkaribisha Lowassa awasalimie kisha mkutano ufungwe, watu watawanyike kwa sababu ya usalama wao.

Ahadi ya Lowassa

Aliposimama kuzungumza, Lowassa alisema alitumia muda mfupi kutoa ahadi zake kwa Wanatanga, na kubainisha kuwa kutokana na hali halisi ni wazi kwamba akizungumza zaidi watu wanaweza kufa na yeye asingependa hali hiyo itokee.

“Ninaomba nimalizie kwa kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi, mkutano huu unanikumbusha nilipokuwa Tanga kuomba sahihi kwenye kura za maoni za CCM..hii ni ishara kwamba mabadiliko ni lazima,” alisema.

Kabla ya kumaliza mkutano huo, Lowassa alisema akichaguliwa kuwa rais atahakikisha katika kipindi cha miezi sita bandari mpya ya Ndumi, itaanza kujengwa kwa sababu wenye uwezo wa kuijenga wapo, lakini Serikali ya CCM inawabania kwa sababu haitaki wananchi wa Tanga wainuke kiuchumi.

Mgombea huyo alisisitiza kuwa sambamba na bandari, akiingia madarakani atasimamia ujenzi wa reli ya Tanga-Arusha-Musoma hadi Kampala, Uganda kwa haraka zaidi kwa kuwa itaharakisha maendeleo.

Mgeja na ahadi za Kikwete

Kabla ya Lowassa kuwasili, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja alisema mikoa ya Tanga na Shinyanga ni waathirika wakubwa wa ahadi alizotoa Rais Jakaya Kikwete wakati akiomba urais, lakini hakuzitekeleza.

Alisema aliahidi kufufua viwanda, kujenga bandari mpya ya Ndumi na kuboresha hali ya wakulima na wavuvi, lakini hadi anamaliza muda wake hakuna hata alichotekeleza.

“Mkiona vigogo wakubwa tumeondoka CCM mjue tumekuja Ukawa kufuata mabadiliko, tumebaini ndani hakuna kitu, kule kumejaa fitina na mizengwe ya kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi, mpeni kura Lowassa na Mussa Mbarouk kwa maendeleo ya Tanga.

Kwa upande wake, Hizza alisema wagombea wa CCM wanaokwenda Tanga kuwaeleza kwamba watafufua viwanda, hawasemi ukweli kwa sababu ndiyo walioviua kwa lengo la kudhoofisha maendeleo ya wana-Tanga.

“Hapa Tanga ni kwetu, hii Tanga haikuwa hivi, wakoloni walijenga reli, bandari, miundombinu mizuri ya mawasiliano pamoja na viwanda ambavyo vilitoa ajira nyingi, lakini CCM imeviua halafu wanaahidi kuvifufua huku ni kuchezeana shere,” alisema Tambwe.

Lowassa awashangaa JK, Pinda

Akiwa Bumbuli, Lowassa ameshangazwa na Rais Jakaya Kikwete na Serikali, kushindwa kutatua mgogoro wa kiwanda cha Mponde ambao umedumu kwa muda mrefu sasa.

Lowassa alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Soni ambao walimweleza kuwa bado wana tatizo la mgogoro wa kiwanda hicho.

“Nashangaa Rais Kikwete, waziri mkuu, mkuu wa mkoa kushindwa kutatua tatizo la kiwanda cha Mponde, hiki kitu gani! Serikali gani hii isiyokuwa na maamuzi,” alisema Lowassa na kuongeza:

“Nisikilize kwa makini, nimechoka, nimechoka kusikia habari za Mponde kila siku halafu hamna suluhisho, kuna nini? Uongozi gani huu unaoshindwa kutatua matatizo madogo kama haya kwa wananchi.

“Ninawahakikishia ndani ya miezi sita nitakuwa nimemaliza suala la Mponde, uongozi wa nchi unahitaji uthubutu, fanya maamuzi hata ukikosea potelea mbali,” alisema.

Septemba 2014, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliagiza wakala wa wakulima wadogo wa chai pamoja na Bodi ya Chai nchini, kuunda timu ya watu wawili au watatu itakayosimamia mwenendo wa kiwanda hicho cha kusindika chai.

Baada ya waziri mkuu kutoa agizo hilo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika ziara za chama jimbo la Bumbuli, Septemba mwaka jana aliwaambia wananchi hao kuwa Rais Kikwete amekirejesha kiwanda hicho kwa wananchi baada ya kuwapo kwa mgogoro uliodumu kwa miaka kumi.

Hata hivyo, jana wananchi wa Bumbuli walionyesha kuwapo kwa mgogoro unaoendelea kuhusu kiwanda hicho, jambo ambalo lilimshangaza Lowassa na kuahidi akiingia madarakani Serikali yake itatatua mgogoro wa kiwanda hicho ndani ya miezi sita.

Pia Lowassa aliwaahidi wananchi hao kuwaondolea umaskini ambao umekithiri kwa kuhakikisha elimu inakuwa bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu ili wananchi wajiendeleze.

Bango la Magufuli lazua kizaazaa

Katika mkutano huo uliofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kisiwani polisi waliwadhibiti vijana watatu waliokuwa wakipita pembeni ya uwanja wakiwa wamebeba bango lililoandikwa ‘Hapa Kazi Tu’.


Pia polisi iliwadhibiti wanawake wawili ambao walikuwa wakipiga kelele katikati ya uwanja huku mmoja akionekana kama amelewa, ambao waliingizwa kwenye gari la polisi na kupelekwa kituoni.

Wananchi walilizingira gari la polisi wakitaka waachiwe watu hao wawashughulikie, lakini askari walifanikiwa kuondoka nao.

Awali, mgombea ubunge wa jimbo la Bumbuli kwa tiketi ya Chadema, David Chinyegheya alidai kulikuwa na vijana wameandaliwa kuvuruga mkutano huo, hivyo aliomba polisi kuwadhibiti.

Imeandikwa na Boniface Meena, Burhan Yakub na Maimuna Msangi.

MWANANCHI