Haya ni maneno ya Idris Sultan kuhusu ujio wa TV Show yake mpya BET…!


Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani… baada ya kuiwakilisha #255 vizuri kwenye shindano hilo kubwa la Africa,mafanikio mengi yamekuwa yakimfuata nyuma Idris Sultan!
SULTAN5
Idris Sultan.
Kama wewe ni miongoni wa watu wanaompenda na kumfuatilia Idris kwenye social networks basi hii good news ikufikie popote ulipo mtu wangu… Idris Sultan siku chache zilizopita alitudokeza kuhusu ujio wa TV Show yake mpya itakayo kuwa inaonyeshwa moja kwa moja kupitia channel ya BET pamoja na channel ya Vuzu za South Africa! Yote ikiwa ni sehemu ya kufanikisha ndoto zake kubwa za kwenda HollywoodMarekani.
SULTAN
Idris kwenye kipindi cha Mkasi.
Staa huyo wa Tanzania ambae pia ni mchekeshaji mzuri sana alipata time ya kupiga stori na millardayo.com kuzungumzia nini kilimsukuma kuja na TV Show yake…
>>> “Kwanza niliwekwa kwenye auditions ambazo nilitakiwa kufanya ili kuingia kwenye Tv show ya ‘The Real Husbands of Hollywood’ show ambayo Kevin Hart yupo, na auditions zangu zilitakiwa zifanyike tarehe 26th April… sasa nikachelewa kuapply Visa ya kwenda USA kwasababu nilikuwa nafanya tours nyingi ndani ya Africa bado kitu kilichopeleka auditions zangu kuwa cancelled, chance hiyo ikanipita na hapo ndipo niliposukunwa sasa kuanzisha reality show yangu mwenyewe ili iwe rahisi kwa mimi kuonekana tena na kupata nafasi nyingine ya kuingia Hollywood…” <<< Idris Sultan.
SULTAN3
Sikuishia hapo, nikamuuliza Idris reality show yake itakuwa inahusu nini na kama show hiyo haitaathiri ndoto zake za kuwa Mchekeshaji mkubwa duniani…
>>> “Reality show hainibadilishi mimi kama mimi kwasababu kwanza haina script, hiyo show itakuwa inaonyesha sana sana ninachokifanya, kwa mfano sasa hivi mnaona tu nafanya vitu tofauti lakini kupitia Reality Show yangu mtakuwa mnaviona ninavyovitimiza, nimevifanyaje, nimepitia nini, na pia muda gani niliwachekesha watu nusu kuzimia… vitu vyote hivi vitaonyeshwa, so kwa ufupi itakuwa inaonesha maisha yangu halisi haswa upande ambao hamuuoni nyinyi kila siku… na haitanipotezea muda bali itakuwa inaonyesha hustle yangu yote na vitu gani ambavyo navifanya mimi kama mimi, na comedy itakuwemo humo humo haitaathiri chochote, comedy zangu zote nitazifanyia humo humo!” <<< Idris Sultan.
SULTAN2
Kama unakumbuka vizuri mtu wangu kuna kipindi Idris alianzisha kitu kinachoitwa‘Hustle & Fame’ kwenye page yake ya Instagram, na inawezekana wengi wetu tumeona lakini hatujui ina maanisha nini… nikamuuliza Idris kama hili ndio jina la show yake mpya?, kwenye kupiga stori, staa huyo aliniambia haya…
SULTAN7
Kwenye show mpya ya Idris Sultan tegemee kukutana na hawa watu mtu wangu, Samantha kutoka South Africa na  Luis Munana kutoka Namibia wote kutoka BBA 2014.
>>> “Yea Reality Show itaitwa ‘Hustle & Fame’ na hilo jina hatukulipata kirahisi kwa sababu tulihangaika sana kama siku nne hivi tunatafuta tu jina, pia tulikuwa tunatafuta jina la show litakaloendana na uhalisia wa maisha yetu sisi ya kila siku tukiwa tayari maarufu lakini bado tunahangaika…” <<< Idris Sultan.
sultan8
>>> “Tumeshafanya asilimia kubwa ya vitu tayari, kama episode 4 za mwanzo tayari tumeshashoot, tunasubiri tu kukamilisha vitu vidogo kama kusign mikataba na BET kama wakiipokea, hoteli tutakazotumia, makampuni ya ndege kwa ajili ya usafiri wa hapa na pale…” <<< Idris Sultan.


x

;

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »