Kauli 8 za Wanawake Ambazo zina maana Kubwa Kwako wewe Mwanaume ila Hujui




1. Mwanamke anaposema, ‘sasa hivi’ au
‘dakika moja tu,’ maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke
sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi
kuliko ule anaoutaja. kama akisema , ‘nusu saa tu, naja,’ unapaswa
kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua
kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri
hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
2. Mwanamke anaposema, ‘utajua
mwenyewe,’ ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia
yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni
sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia
hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana
ingawa siyo lazima.

3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani
kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama
anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa
kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba,
haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo
la maana unalomweleza.

4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole,
ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani,
ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo
yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza
kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha
pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa
wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona
hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole,
hukuona ‘babu kubwa’ kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo
tu.

5. Mwanamke anapotumia neno, ‘sawasawa,’
kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, ‘ninachukua
muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.’ Kauli hii siyo
nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa
visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri
kuambiwa,’sawasawa,’ au ‘sawa bwana,’ kabla ya visasi hivyo.

6. Mwanamke anapotamka neno, ‘we endelea
tu,’ anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo
ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye
kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa
pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na
tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.

7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema,
‘sawa bwana fanya,’ kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au
amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana
maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini
kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.

8. Je kama mmeshindana katika jambo au
umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo
fulani, halafu akakumabia, ‘asante sana,’ itakuwa na maana gani? Hii ina
maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni
toafauti na ‘asante’ ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno ‘sana,’ujue
umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema,
‘asante sana,’ anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora
unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza


x

;

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »