MAGEUZI! Mama mzazi wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ametoa baraka kwa bintiye huyo ambaye kiimani ni Mkristo, kufunga ndoa ya Kiislam kwa madai kuwa ndoa si dini bali ni utu wa mtu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kuna barua za posa mbili ambazo mwanamke huyo mwenye misimamo amekuwa akizikataa kutokana na wahusika kuwa na imani tofauti na Lulu.
Staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na mamaake.
CHANZO CHAANIKA MSIMAMO WA MAMA LULU
“Unajua mama Lulu ni mwanamke mwenye misimamo sana. Akishikilia jambo kashikilia. Posa mbili zilishafika akagoma katakata, kisa waoaji si Wakrsito. Lakini hilo nalo limeonekana kumuumiza kisaikolojia Lulu maana hajui ni mwanaume gani aliyepangiwa na Mungu.
“Watu wengi wamekuwa wakimlaumu sana mama Lulu wakidai kuwa anakataa posa za wanaume wa Kiislam kwa kigezo cha dini lakini kumbe anataka tu akae na mwanaye pale nyumbani.”
“Ninavyojua mimi, kikubwa kilichokuwa kikimfanya mwanamke huyo ashikilie msimamo huo ni historia yake. Anasema katika ukoo wake na wa baba Lulu (Michael Kimemeta) hakuna Muislam (mwanaume) aliyeoa hapo wala Mkristo (mwanamke) aliyekwenda kuolewa na Muislam,” kilisema chanzo.
...Baba Lulu.
MAHOJIANO
Amani lilimuuliza kama miongoni mwa wachumba wawili waliojitokeza kumchumbia Lulu wakakataliwa, yupo staa wa sinema za Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye hivi karibuni aliripotiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kuwa siku hizi yupo ‘vere klozdi’ na Lulu, mahaba yakatajwa, lakini alitoa majibu ya njia panda bila kusema ni kweli au kinyume chake!
Chanzo: “Sina hakika. Ila wapo wawili. Nadhani mama Lulu mwenyewe anajua. Nendeni mkazungumze naye. Ila ni mtata sana yule mama, si wa kumwingia kirahisirahisi tu.”
Amani: “Kwani Lulu mwenyewe alikuwa tayari kuolewa Kiislam?”
Chanzo: “Inasemekana yeye yuko tayari.”
KUHUSU BABA LULU
Amani lilimuuliza mtoa habari huyo kama anajua msimamo wa baba Lulu kuhusu mwanaye kubadili au kutobadili imani.Chanzo: “Unajua yule mzee ana maisha yake kwa sasa. Ana familia yake. Lulu ni mwanaye lakini naamini mwongozo mkubwa anaupata huku Dar kwa mzazi mwenzake (mama Lulu).”
Dk. Cheni.
MAMA LULU ASAKWA
Juzi, Amani lilimsaka mama’ke Lulu na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo mahojiano yake na paparazi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
“Labda niseme kwanza mimi mtoto wangu hajawahi kuletewa posa nyumbani, isitoshe hata yeye mwenyewe hajawahi kuniletea mchumba na kuniambia kuwa anataka kumuoa.
“Awali nilipenda mtoto wangu aolewe na mtu wa imani yake kwa sababu yeye mwenyewe amekulia katika Ukristo mpaka kufikia hapa alipo sasa.“Lakini siku hizi wazazi wanaangalia utu wa mtu na vitu vingine vinakuja baadaye kabisa, kwa vile anaweza hata akaolewa na mwanaume wa dini yake bado akamletea shida maishani.
“Ngoja nikwambie, kwanza sidhani kama sasa hivi mapenzi yanaangalia dini wala kabila. Kama yeye atamleta Muislam na kampenda kutoka kwenye moyo wake na mimi nitampokea wala sitakuwa na pingamizi lolote.
AMANI LARUDI KWA DK. CHENI
Baada ya Amani kumalizana na mama Lulu, lilirudi kwa Dk. Cheni anayetajwa hivi karibuni ‘kutoka’ na Lulu ambapo aliulizwa kwa staili kuwa, wasomaji wa gazeti hili wanataka kujua kama kweli atamuoa Lulu. Alijibu:
“Swala la kutomuoa au kumuoa Lulu ni langu binafsi. Hebu subirini msiwe na haraka mtakuja kuujua ukweli. Mbona Watanzania mlio wachache mnakosa uvumilivu? Yaani mnapenda kujua mambo ya mbele kabla wakati haujafika.
“Hebu kaeni chini mtafakari nchi ya Japan wanatengeneza magari lakini nyie hata baiskeli hamuwezi. Tafakarini ubunifu wenu siyo mambo ya watu.”
Amani lilimkosa Lulu hewani lakini maelezo ya mama yake kama mkuu wa familia yalitoa picha ya msimamo kuhusu binti huyo ambaye hivi karibuni aliripotiwa kujikita kwenye maombi kwa kusali na kumwabudu Mungu katika roho na kweli japo mara kadhaa amewahi kunaswa akipombeka kama ishara ya shetani kumzidi mabavu.
Chanzo:GPL
;