Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya kuitwa Msaliti aliposhindwa kutoka Nje ya Bunge



Jana Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilifungua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) walipiga kelele na kutolewa na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai katika kushinikiza kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein, ila Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe hakutoka nje na Baadhi ya watu kutafsiri kuwa aliwasaliti wabunge wenzake wa Upinzani, Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Zitto Kabwe alipost habari yake kuhusiana na tukio hilo. Na hiki ndicho alichokipost;

"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake. Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia. Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa. Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma."


x

;

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »