WAKATI kukiwa na kashfa nzito kuwa wanawake mbalimbali wakiwemo, wasanii wa wakike nchini Tanzania, kujihusisha na tabia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, Lulu Mathias Semagongo maarufu kwa jina la ‘Aunt Lulu’ amevunja ukimya na kutangaza wazi kwamba aliwahi kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Lulu ametoa siri hiyo baada ya kumtuhumu msanii wa filamu Wastara Sajuki,kwamba anatumika kinyume na maumbile tangu mumeweJuma Kilowoko (Sajuki) alipofariki dunia, Lulu alitoa kashfa hiyo baada ya kubaini kwake Wastara ameanza kuwa na mahusiano ya mapenzi na msanii mwenzake, Bond Bin Suleiman, ambaye aliwahi kuwa na mahusiano na Aunt Lulu.
Aunt Lulu alidai kwamba Bond anatabia ya kula nyuma na mbele tena kwa kulazimisha na wakati mwingine anatumia hata dawa za kelevya kwa kumpa mwanamke, ili atimize hazma yake.
Aunt Lulu akiwa katika moja poz zake ndani ya bwawa la kuogelea
Akizungumzia sakata hilo Aunt Lulu alisema kwamba wakati akiwa kwenye mapenzi na Bond alishindwa kuvumilia ujinga wake na akalazimika kujiondokea kwa sababu si mwanaume mwenye maadili ya mapenzi.
Baada ya kuona Wastara wamepuuzia tuhuma na hizo huku akizidisha manjonjo kwa Bond, Lulu ameamua kuweka siri yake wazi kwamba amewahi kufanya mapenzi kinyume na maumbile akiwa na mwanaume wa kizanzibari, akihojiwa na gazi moja la udaku la kila wiki nchini Tanzania Lulu alisema kwamba yeye amewahi kujihusisha na mchezo huo' “Mimi sipendi kabisa, ila iliwahi kunitokea mara moja kipindi nilipokuwa na bwana wangu wa Kinzanzibari.
“Kwa kweli ni mateso makubwa. Kwanza yule mwanaume alinibaka, haikuwa ridhaa yangu na kunitenda hivyo nilimuacha. Nawaomba wengine waelewe kuwa ni jambo baya. Binafsi sitakuja kufanya katika maisha yangu yote.”
Kuhusu idadi ya wasanii wanaotuhumiwa kujihusisha na mchezo huo; Lulu aliendelea kusema: “Mimi nina orodha ndefu ya mastaa wanaojihusisha na tabia hiyo, siwataji kwa sasa lakini zaidi ya asilimia 90. Unajua hivi sasa hata wanaume wanaotendwa mchezo mchafu ni wengi ndiyo maana wanawake wanaamua kuachia ili wasizidiwe kete na wanaume mashoga.”
;