Showing posts with label Aunt Ezekiel. Show all posts
Showing posts with label Aunt Ezekiel. Show all posts

Aunt Ezekiel: Nimeamua Kuhama CHADEMA Na Kurudi CCM Baada ya Kuvutiwa na Sera za Chama........Sijapewa Pesa wala Gari


MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka CHADEMA  na kwenda CCM.

Licha ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama chama hicho na kujiunga na CCM kutokana na kukubali sera za chama hicho.

“Sera za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala sijapokea fedha wala gari kuhamia huko kama inavyosemekana, bali nafsi na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.

“Nashangaa maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia kama walivyo wengine, umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda  CHADEMA

Aunty Ezekiel: Ningetaka Mtoto Mweupe Ningezaa na Mzungu


MSANII wa Bongo Movie anayetambulika kwa jina la Aunty Ezekiel amewajia juu mashabiki wake wanaomuongelea vibaya mtoto aliyezaa na mnenguaji wa Diamond Platnumz, Mozee Iyobo.


Aunty Ezekiel aliandika katika mtandao wa jamii kwamba amesikitishwa na namna baadhi ya mashabiki wake wanavyong’ang’ania aweke picha ya mtoto wake anayetambulika kwa jina la Cookie.

“Kuweka uso wa mwanangu mtandaoni ni hiari yangu, msilazimishe, mwanangu ni mweusi sana au ana chongo siwezi kumuanika hadharani, mimi ndiye najua utamu na uchungu wake, ningetaka kuzaa mtoto mweupe ningezaa na mzungu,’’ aliandika Aunty Ezekiel.

Chanzo:Mtanzania