Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts
Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts

Wema Sepetu Atoboa Siri...Aliyekuwa Mume wa Zari Anamtongoza na Ahadi ya Kumuoa

 
Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa.
Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu.
“Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.”
“Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwishoni ilibidi tuwakubalie lakini kwa masharti ya kuwa wasije wakatuzushia lolote.
“Tulikubali, wakaja, tukakaa nao meza moja, tukabadilishana mawasiliano kama marafiki. Lakini baadaye tukaona wanaongezeka, sikupenda vurugu ya watu wengi, mimi na Ommy tukaamua kuondoka zetu,” alisema Wema.
Akizidi kumwaga siri zake na mwanaume huyo, Wema alisema baada ya yeye kumaliza project yake nchini humo, alirejea Bongo na ndipo Ivan alipozidisha ufundi wa kumuomba urafiki wa kimapenzi huku akimuahidi mambo mengi ya muhimu.
Msikie Wema: “Baada ya hapo tulikuwa tunawasiliana na Ivan, lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, nikaona mwenzangu anaanza kunitongoza, tena akawa anaendelea kila siku licha ya mimi kutomkubalia.”

Aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga.
Wema alizidi kutiririka kuwa, hadi sasa (mapema wiki hii), Ivan hajakata tamaa, amekuwa akiendelea kumtongoza na kumuahidi ahadi mbalimbali.
Endapo atamkubalia na kuwa baby wake, basi atampa nyumba ya kifahari na magari ya kisasa (awe kama Zari).
Wema anakiri mwenyewe: “Alianza kuniahidi maisha mazuri, nyumba, magari na hata kunioa lakini kimsingi sijamkubalia kwani sijamwamini kama ana mapenzi ya dhati. Nahisi kuna kitu nyuma yake kinamsukuma kufanya hivyo.”
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa Wema akaingia kwenye himaya ya Ivan kutokana na ushawishi wake mkubwa anaoufanya kwa madam huyo, hivyo akawa tajiri mkubwa.
“Wema kwa sasa hatakiwi kuichezea bahati kwani Ivan ni mtu anayejiheshimu. Ana biashara zake kubwakubwa, hivyo suala la fedha za maisha hazimpigi chenga,” kilisema chanzo hicho. Akizungumzia suala hilo, rafiki wa karibu wa Wema ambaye hakupenda jina lake liandikwe , alisema licha ya Wema kutokubali ombi la Ivan lakini anaamini siku si nyingi atakubali na atakuwa vizuri kiuchumi kuliko alivyo sasa.
“Jamaa yupo serious na ndoa, Wema atakubali tu na ndoa itafungwa. Mtoto wa kike sasa atakuwa si wa magari ya kawaida, full kubadilisha, atakuwa mtamu kama mcharo,” alisema rafiki huyo.
Rafiki huyo aliendelea kusema kuwa, Wema ana wasiwasi kwamba, mapenzi ya Ivan kwake ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa sababu ya Diamond (aliyekuwa mpenzi wa Wema) sasa yuko na Zari (aliyekuwa mke wa Ivan).
“Kwa hiyo Wema ana wasiwasi kwamba, siku akimkubalia tu Ivan akapiga naye ngwara, biashara itakuwa imeishia hapo kwani nia ya kisasi ya mwanaume huyo itakuwa imekamilika,” alisema rafiki huyo.

Picha za WEMA SEPETU akiwa katika Instagram Party Jijini Mwanza

 
Usiku wa tarehe 27, ulipambwa na Show ya Instagram Party kwa upande wa Mwanza 88.1, mastaa kadhaa wa Tanzania walikuwepo kunogesha Party kutoka Bongo movie Wema Sepetu, alikuwepo na kundi la Weusi liliwakilishwa na Joh Makini pamoja G nako.Party imefanyika Rock City Shopping mall Mwanza.
 
 
 
Eti Wema, Aunt wapatana!

Eti Wema, Aunt wapatana!

IMG-20151214-WA0004
Waigizaji wa filamu wenye majina makubwa Bongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel katika pozi.

KITUKO! Katika hali isiyotarajiwa, waigizaji wa filamu wenye majina makubwa Bongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamepatana ghafla baada ya ugomvi wao wa muda mrefu.

Katika akaunti zao za mitandao ya kijamii, wawili hao walitupia picha wakiwa pamoja na furaha tele, baada ya hafla ya kukabidhiwa tuzo kwa wasanii zinazojulikana kama Nzumari Awards 2015, zilizofanyika Mombasa nchini Kenya, Ijumaa iliyopita.
IMG-20151214-WA0005
Inafahamika kuwa waigizaji hao wamekuwa katika ugomvi mkubwa ambao chanzo chake hakiwekwi wazi, lakini mara kadhaa, wameshindwa kuhudhuria hafla zilizowahusisha wao au familia zao na kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipondana.

Chuki kubwa zaidi ya hivi karibuni ni pale Aunt Ezekiel alipompigia ‘promo’ Diamond katika pati yake ya Zari White Party iliyofanyika Mei mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jambo ambalo lilimkera Wema, aliyetemana na mkali huyo wa kibao cha Mdogomdogo.
Cha kushangaza zaidi, alipoulizwa kama wamepatana lini, Aunt Ezekiel, aliyezaa na dansa wa Diamond, Mose Iyobo alisema; “Kwani tulikuwa tumegombana jamani? Mimi hayo mambo nilikuwa ninasoma kwenye magazeti tu, sisi hatujawahi kugombana hata mara moja.”
Pacha wa Wema ni gumzo!

Pacha wa Wema ni gumzo!

turwema
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na pacha wake.
Ule msemo kwamba duniani ni wawiliwawili umeonekana kuwa na nguvu baada ya kuwepo kwa binti mrembo anayefanana sana na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
turwe6
Binti huyo anayefahamika kwa jina la Tuerney ambaye pia ana shepu bomba, amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook kwani wadau wamekuwa wakiweka picha zake na za Wema kisha kuonesha jinsi walivyofanana.

Ijumaa lilifanya jitihada za kutaka kumjua kwa undani lakini katika kuonesha si mtu wa kutaka umaarufu kivile, alipotafutwa alikataa kutoa ushirikiano akisema yeye hataki mambo ya magazeti. Jionee picha!
Zari atumika kumdhalilisha Wema...Kisa kuzaa na Diamond Platnumz!

Zari atumika kumdhalilisha Wema...Kisa kuzaa na Diamond Platnumz!

zarinah
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’

WATU wabaya! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia watu wanaoasadikiwa kuwa ni wafuasi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutumia jina na picha ya mwandani wa sasa wa staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumdhalilisha mpenzi wa zamani wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tangu Zari, ambaye ni mjasiriamali maarufu aliyemzalia Diamond, amfanyie mwanaye Latiffah ‘Tiffah’ sherehe ya kumtoa nje kwa mara ya kwanza (Arobaini).
ZARI (1)
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
KIINI CHA UDHALILISHAJI
‘Kirusi’ wa kwanza kuanzisha udhalilishaji huo alijitambulisha katika mtandao wa Instagram kwa jina la Who is Boss ambapo aliweka picha inayomuonyesha Zari akiwa amembeba mtoto wake na Wema akiwa amembeba mbwa kisha kusindikiza ujumbe uliosomeka:
“Ukibeba mimba utalea mtoto na ukitoa mimba utalea mbwa.”
TIMU DIAMOND ZAMSHAMBULIA WEMA
Mara baada ya Who is Boss kuweka picha na ujumbe huo, wafuasi wa Diamond (Team Diamond) walianza kumshambilia Wema kwa kumkejeli na kumtukana matusi mazito yasiyoandikika gazetini.
Wafuasi hao walimtuhumu Wema kuwa alichezea ujana kwa kutoa mimba matokeo yake kwa sasa analea mbwa wakati mwenzake Zari ametumia ujana wake vizuri na ndiyo maana amemzalia Diamond.
wema (3)
Wema Sepetu ‘Madam’.
WEMA ABUBUJIKWA MACHOZI
Chanzo kilicho karibu na Wema kilipenyeza habari kuwa alipopewa taarifa hizo za kudhalilishwa mtandaoni, alisikitishwa na kejeli hizo kiasi cha kumwaga machozi kwani suala la kutopata mimba yeye linamtesa hivyo mtu anapomkejeli, anaumia sana.
“Huwezi amini Wema amemwaga machozi. Anaumizwa sana na hawa watu wanaomkejeli kila kukicha mitandaoni hususan katika suala linalohusu mtoto,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambaye alikiri kukejeliwa na kusema ameumizwa na taarifa hizo hivyo analiomba jeshi la polisi nchini kuwashughulikia watu hao kupitia sheria mpya ya mtandao.
“Sijam-follow huyo mtu, ninapewa taarifa na watu, naamini atapatikana tu tena siku si nyingi maana watu wanapenda kutukana wenzao bila sababu za msingi,” alisema Wema.
MAMA WEMA ACHARUKA
Mbali na Wema, udhalilishaji huo ulimtibua mama mzazi wa staa huyo, Miriam Sepetu ambaye alisema hawezi kuacha suala hilo lipite hivihivi, atahakikisha ‘anadili’ na watu wote wanaomuandama mwanaye mitandaoni na kwa kuanzia watamshtaki Who is Boss.
“Hata siku moja sio haki kwa kweli, huwezi mtu ukasema kuwa analea mbwa na wakati hakuna hata mtu mmoja aliyempima mtoto wangu  na kujua hawezi kuzaa mtoto kwa hili sitokaa kimya nitamshtaki na piga ua, atapatikana tu,” alisema mama Wema.
AZIDI KUTIRIRIKA
Mama huyo alienda mbele zaidi na kusema kumekuwa na vitu vingi ambavyo vimekuwa vikimdhalilisha mwanaye na kumletea picha mbaya katika jamii, hivyo mamlaka zinazohusika na mitandao zinabidi zichukue hatua stahiki.
“Kwa hili sitanyamaza na itakuwa mfano maana watu wamezidi kudhalilisha   wenzao, TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) lazima ianze kufanya kazi yake na iwe fundisho,” aliweka nukta Mama Wema.

Chanzo: GPL