Showing posts with label Lowasssa. Show all posts
Showing posts with label Lowasssa. Show all posts
Hizi ndizo Siri za Ushindi wa Edward Lowassa!

Hizi ndizo Siri za Ushindi wa Edward Lowassa!

lowassaa
Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

MGOMBEA urais wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ana nafasi ya kuibuka na ushindi wa kiti cha urais iwapo chama hicho kitaongeza juhudi katika mkakati wa kuwafikia wananchi wengi zaidi maeneo ya vijijini katika siku zilizobaki, Uwazi Mizengwe limefahamishwa.
Wachambuzi wa masuala ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliliambia gazeti hili kuwa Lowassa ni mwanasiasa mwenye mvuto na ushawishi mkubwa kwa wananchi, hivyo iwapo atatumia vyema siku zilizobaki kuwafikia wananchi wengi zaidi, ana uwezo wa kuibuka mshindi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Hata hivyo, wanazuoni hao walitoa angalizo kuwa mkakati huo hauwezi kufanikiwa iwapo Chadema itaendelea na mkakati wake wa kutumia usafiri wa helikopta kwa kuwa mgombea wao hatakuwa na fursa pana ya kukutana na wapiga kura.
“Lowassa amekuwa akitumia helikopta katika kampeni lakini ikumbukwe kwamba kwa kutumia usafiri huo, hawezi kuwafikia wananchi wengi kama mgombea anayetumia barabara kwa kuwa Anakutana na wapiga kura wengi zaidi ambao anaweza kuwabadili fikra na mtazamo hatimaye kumuunga mkono,” alisema Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.
Pia alisema kuwa Lowassa amekuwa akitumia mkakati wa kuteka saikolojia ya watu kwa ahadi ya kuwaondolea umaskini wananchi hasa akina mama na vijana, mkakati ambao ni muhimu kwa kuwa hilo ndilo kundi kubwa la wapiga kura, hali inayompa taswira ya ushindi kutokana na kuungwa mkono na makundi hayo.
Walisema kwamba iwapo CCM isipowafikia wananchi wengi zaidi na kunadi sera zake na kuwapiga propaganda ili kuwashawishi kuondokana na itikadi za mabadiliko zinazonadiwa na Chadema, inaweza kusababisha chama hicho kikakosa ushindi.
Hata hivyo, walisema kuwa chama hicho kina uwezekano mkubwa wa kushindwa katika uchaguzi huo iwapo mgombea wake (Lowassa), ataendelea na tabia yake ya kutojinadi kwa muda mrefu, kwa kuwa wapiga kura wanamhusisha na magonjwa, jambo ambalo limekuwa likishusha morali ya kumpigia kura katika uchaguzi ujao Wakati huohuo, walisema mkakati wa Chadema wa kueneza propaganda kupitia mitandao ya kijamii unampa Lowassa nafasi kubwa ya kuungwa mkono hasa katika maeneo ya mijini, hivyo anaweza kujikuta akipata kura nyingi katika maeneo hayo ikiwa CCM isipokuwa makini kujibu mashambulizi ya propaganda hizo.
Hata hivyo, wataalam hao walifafanua kuwa CCM ndiyo chama kinachofanya kampeni za uhakika zaidi kutokana na mkakati wake wa kuzunguka nchi nzima kwa kutumia barabara hivyo kitawafikia wapiga kura wengi zaidi kuliko chama chochote cha siasa nchini kinachowania nafasi hiyo.
Walisema kuwa kutokana na mkakati huo, Magufuli ndiye mgombea anayeungwa mkono na watu wengi zaidi nchini na kuongeza kuwa CCM inajiimarisha zaidi siku zilizobaki kuhakikisha kwamba inapata ushindi mnono dhidi ya Chadema.
Waliongeza kwamba CCM imeelekeza zaidi kampeni zake katika maeneo ya vijijini ambako kuna zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura ambao wengi wao si watumiaji wa mitandao ya kijamii. Waliongeza kuwa mtaji mkubwa wa CCM wa wanachama zaidi ya milioni 6, unakipa chama hicho uhakika zaidi wa kuibuka mshindi kutokana na uhamasishaji unaofanyika kuanzia katika kaya hadi ngazi ya taifa.
alifafanua kuwa pamoja na mtaji huo, Magufuli kupitia mikutano yake ya kampeni amekuwa akitumia muda mrefu zaidi kunadi sera za chama chake na kueleweka zaidi kwa wapiga kura kuliko Lowassa ambaye amekuwa akitumia muda mfupi kuzungumza katika mikutano yake.

LOWASA azidi kuunguruma kwenye Kampeni Zake...Safari hii ndani ya Kigoma!

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Kigoma Kusini, waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

Baadhi ya wananchi wa Mji wa Kigoma Kusini, wakionyesha furaha yako kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.


 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akikaribishwa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe. Picha na Othman Michuzi, Kigoma.










Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Jimbo la Kigoma Kusini, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

LOWASSA kuanza kuwasha Moto Rasmi Kesho Jangwani


MRATIBU wa Maandalizi ya Kampeni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Deogratia Munishi amesema maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni yamekamilika kwa asilimia 90.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja hivyo vya Jangwani, Munishi amesema kila kitu kipo tayari katika maandalizi hayo na wanachosubiri ni mkutano.

Munishi amesema mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni umepangwa kuanza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.

Amesema, mkutano utahudhuliwa na watu kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwemo wanachama kutoka nje ya nchi kama Zambia na sehemu nyingine duniani.

Aidha, amewataja viongozi watakaohutubia katika mkutano huo kuwa, Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, Mgombea Mweza, Juma Duni Haji, viongozi wakuu wa UKAWA na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali.

Kuhusu uwepo wa wasanii katika mkutano huo amesema: “Wasanii watakuwepo lakini hawatapamba mkutano kama kule kwa wenzetu, sisi tunakuja kutangaza sera na sio tamasha la wasanii.”

Naye Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ametoa ratiba ya Mgombea urais na mgombea mwenza kuwa, mara baada ya uzinduzi wa kampeni hizo wataanza ziara mikoani.


Amesema Lowassa, Jumapili ataanza ziara yake Mkoani Iringa na kufanya mikutano ya hadhara minne ambapo ataanzia Mufindi, Kilolo, Karenga, na Iringa Mjini kila sehemu mkutano mmoja.

Kwa Upande wa Babu Duni, amesema ataanzia Mtwara katika wilaya ya Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na Mtwara mjini.

Aidha, kuhusu tetesi za uwepo wa Katibu mkuu Chadema, Dk. Willbrod Slaa viwanja vya jangwani Makene amesema: “Hizo ni tetesi tu. Hakuna ukweli wowote. Dk. Slaa (Willbrod) amepumzika acheni kumzushia maneno.”

Ameongeza, mkutano utakuwa laivu katika televisheni na radio zisizopungua tano kuanzia saa 9 hadi 12 jioni.


Ratiba ya Kampeni ya EDWARD LOWASSA hadi kufikia siku ya Uchaguzi Oktoba 25



CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
RATIBA YA MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 2015
tarehe mkoa wilaya muda maelezo
29/8/2015 Dar es salaam wilaya zote saa 1.00 asubuhi hadi 12.00 jioni uzinduzi wa kampeni kitaifa
Iringa 
30/08/2015 Mufindi saa 3.00 hadi saa 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mufindi mjini 
Kilolo saa 5.30 hadi saa 7.00 mchana mkutano utafanyika ilula
isimani na
Kalenga saa 8.00 hadi saa 9.30 alasiri mkutano utafanyika kalenga
Iringa mjini saa 10.30 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika mwembetogwa/mlandege
31/08/2015 Njombe Makambako saa 3.00 hadi saa 4.30 asubuhi mkutano utafanyika makambako
Ludewa saa 5.30 hadi saa 6.30 mchana mkutano utafanyika ludewa mjini
Njombe Kusini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika njombe mjini
1/09/2015 Ruvuma Peramiho saa 3.00 hadi saa 4.30 asubuhi mkutano utafanyika madaba
Nyasa saa 5.30 hadi saa 6.30 mchana mkutano utafanyika nyasa
Mbinga saa 8.00 hadi 9.00 alasiri mkutano mbinga mjini
Songea saa 10.30 hadi saa 12 jioni mkutano songea mjini
02/09/2015 Tunduru saa 3.00 hadi saa 4.30 asubuhi mkutano tunduru
namtumbo saa 5.30 hadi saa 7.00 mchana mkutano namtumbo mjini
02/09/2015 rukwa sumbawanga saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano sumbawanga mjini
03/09/2015 nkasi saa 3.00 hadi saa 4.30 asubuhi mkutano utafanyika namanyere
03/09/2015 katavi mlele saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika mlele
mpanda saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika mpanda mjini
04/09/2015 kigoma uvinza saa 3.00 4.30 asubuhi mkutano utafanyika uvinza
kigoma vijijini saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano kigoma kaskazini
kigoma ujiji saa 8.30 hadi 10.00 jioni mkutano utafanyika ujiji
05/09/2015 tabora sikonge saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika sikonge mjini
urambo saa 6.00 hadi 7.30 mchana mkutano utafanyika urambo mjini
tabora mjini saa 9.30 hadi saa 12.00 jioni mkutano utafanyika tabora mjini
06/09/2015 nzega saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika nzega mjini
igunga saa 5.30 hadi saa 7.00 mchana mkutano utafanyika igunga mjini
07/09/2015 dar es salaam kinondoni saa 5:00 hadi 7:00 mchana mkutano kufanyika bunju
saa 9:00 hadi saa 12:00 jioni mkutano utafanyika kibamba
08/09/2015 morogoro ulanga saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mahenge
kilombero saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika ifakara
kilosa saa 9.00 hadi 11.00 alasiri mkutano utafanyika mikumi
09/09/2015 kilosa saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika turiani
mvomero saa 5.00 hadi saa 6.30 mchana mkutano utafanyika dumila
morogoro vijijini saa8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika ngerengere
morogoro mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika morogoro mjini
10/09/2015 gairo saa 3.00 hadi saa 4.30 asubuhi mkutano utafnyika gairo
10/09/2015 dodoma kongwa saa 5.30 asubuhi hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika kibaigwa
mpwapwa saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika kibakwe
mpwapwa saa 10.30 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika mpwapwa
11/09/2015 dodoma vijijini saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mvumi
chamwino saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika chamwino
bahi saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika bahi mjini
dodoma mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika dodoma mjini
12/09/2015 kondoa saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika kondoa mjini
singida ikungi saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika ikungu mjini
singida mjini saa 10.30 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika singida mjini
13/09/2015 singida vijijini saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika singida kaskazini
mkalama saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika mkalama
iramba saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika iramba magharibi
14/09/2015 shinyanga kahama saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika kahama mjini
kishapu saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika kishapu
shinyanga vijijini saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika solwa
shinyanga mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika shinyanga mjini
15/09/2015 simiyu maswa saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika maswa mjini
bariadi saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika bariadi mjini
busega saa 9.30 hadi 11.00 jioni mkutano utafanyika busega mjini
16/09/2015 geita mbogwe saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mbogwe
bukombe saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika mbogwe mjini
chato saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika chato mjini
geita mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika geita mjini
17/09/2015 geita saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika busanda
kagera biharamulo saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika biharamulo mjini
ngara saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika ngara mjini
18/09/2015 karagwe saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika karagwe mjini
muleba saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika muleba mjini
bukoba mjini saa 9.00 hadi saa 12.00 jioni mkutano utafanyika bukoba mjini
19/09/2015 nkenge saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika nkenge
misenyi saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika misenyi
bukoba vijijini saa 8.00 hadi 10.00 alasiri mkutano utafanyika bukoba vijijni
20/09/2015 dar es salaam kigamboni saa 3:30 hadi saa 6:00 mchana mkutano utafanyika kigamboni
mbagala saa 7:00 hadi 9:00 alasiri mkutano utafanyika zakhem
ukonga saa 10:00 hadi 12:00 jioni mkutano kufanyika pugu
21/09/2015 mtwara newala saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika newala mjini
tandahimba saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utanyika tandahimba mjini
mtwara vijijini saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika nanyamba
mtwara mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika mtwara mjini
22/09/2015 masasi saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika ndanda
masasi saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika masasi mjini
23/09/2015 lindi liwale saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika liwale mjini
nachingwea saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika nachingwea mjini
kilwa saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika kilwa kaskazini
kilwa saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika kilwa kusini
24/09/2015 lindi vijijini saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mtama
lindi mjini saa 5.30 hadi 7.00 mchan mkutano utafanyika lindi mjini
25/09/2015 pwani mafia saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mafia mjini
rufiji saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika ikwiriori
mkuranga saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika mkuranga mjini
kisarawe saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika kisarawe mjini
26/09/2015 bagamoyo saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika bagamoyo mjini
bagamoyo saa 5.30 hadi 7.00 mchan mkutano utafanyika chalinze mjini
kibaha vijijini saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika mlandizi
kibaha mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika kibaha mjini
27/09/2015 pemba pemba saa 3:00 hadi saa 7:00 mchana mkutano utafanyika tibirinzi

27/09/2015 unguja unguja saa 10:00-saa 12:00 jioni mkutano utafanyika kibanda maiti

28/09/2015 tanga mkinga saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mkinga
muheza saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika muheza
pangani saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika pangani
tanga jiji saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika tanga jiji
29/09/2015 lushoto saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika bumbuli
korogwe vijijini saa 5:30 hadi 6:30 mchana mkutano unafanyika mombo
korogwe mjini saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika korogwe
handeni saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika mkata
30/09/2015 kilindi saa 3:00 hadi 5:00 asubuhi mkutano kufanyika kilindi
handeni saa 5:30 hadi 7:00 mchana mkutano kufanyika handeni
01/10/2015 dar es salaam temeke saa 5.30 hadi 7.00 mchana mwembe yanga
ilala saa 8.00 hadi 9.30 alasiri segerea
kinondoni saa 10.00 hadi 12.00 jioni tanganyika packers

02/10/2015 manyara kiteto saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika kibaya mjini
simanjiro saa 6:00 hadi 8.00 mchana mkutano utafanyika orkesmet mjini
babati vijijini saa 10.00 hadi 12:00 jioni mkutano utafanyika magugu
03/10/2015 babati mjini saa 03.00 hadi 04:30 asubuhi mkutano utafanyika babati mjini
hanang saa 6.00 hadi 8:00 mchana mkutano utafanyika katesh
mbulu saa 10:00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika mbulu
04/10/2015 mwanza magu saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika magu
kwimba saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika ngudu
misungwi saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika furahisha
sengerema saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika sengerema mjini
05/10/2015 ukerewe saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika nansio
ilemela saa 6:00 hadi 07.00 mchana mkutano utafanyika igombe
nyamagana saa 10:00 hadi 12:00 jioni mkutano kufanyika nyamagana
06/10/2015 mara tarime saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika tarime mjini
rorya saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika rorya
bunda saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika bunda mjini
butiama saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika butiama
07/10/2015 serengeti saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika serengeti
musoma mjini saa 6.30 hadi 10.00 alasiri mkutano utafanyika musoma mjini

08/10/2015 arusha ngorongoro saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika sale
ngorongoro saa 6:00 hadi 8:00 mchana mkutano utafanyika loliondo
karatu saa 10:00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika karatu
09/10/2015 monduli saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika mto wa mbu
monduli saa 5:30 hadi 7:00 mchana mkutano utafanyika monduli
longido saa 8.00 hadi 09.30 alasiri mkutano utafanyika longido
arumeru magharibi saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika ngaramtoni
10/10/2015 arumeru mashariki saa 3.00 hadi 5.30 asubuhi mkutano utafanyika usa river
arusha mjini saa 8.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika arusha mjini

11/10/2015 kilimanjaro siha saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika siha
hai saa 5.30 hadi 7.30 mchana mkutano utafanyika hai
moshi vijijini saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika moshi vijijini
moshi mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika moshi mjini
12/10/2015 moshi vijijini saa 3.00 hadi saa 5.00 asubuhi mkutano utafanyika vunjo
rombo saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano utafanyika rombo mjini
mwanga saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika mwanga mjini
same magharibi saa 10.30 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika same mjini
13/10/2015 same mashariki saa 3.00 hadi 5.00 asubuhi mkutano utafanyika gonja
same saa 6:00 hadi 8.00 mchana mkutano utafanyika hedaru
14/10/2015 mbeya momba saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano unafanyika momba
tunduma saa 5.30 hadi 7.00 mchana mkutano unafanyika tunduma
ileje saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano unafanyika ileje
vwawa saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano unafanyika vwawa
15/10/2015 mbozi saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano unafanyika mbozi
chunya saa 9.00 hadi 12. 00 jioni mkutano unafanyika chunya
16/10/2015 mbarali saa 3.00 hadi 5.00 asubuhi mkutano unafanyika mbarali
rungwe m/riki saa 7.00 hadi 9.00 alasiri mkutano unafanyika rungwe mashariki
rungwe m/magh saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika rungwe magharibi
17/10/2015 kyela saa 3.00 hadi 4:30 asubuhi mkutano utafanyika kyela
njombe makete saa 6:30 hadi 8:00 mchana mkutano utafanyika mbeya mjini
mbeya mbeya mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano unafanyika mbeya mjini
18/10/2015 geita geita mjini saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano unafanyika geita
mwanza nyamagana saa 6.00 hadi 8.00 mchana mkutano unafanyika nyamagana
mara butiama saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano unafanyika butiama
19/10/2015 dodoma mpwapwa saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano unafanyika kibakwe
chamwino saa 6.00 hadi 8.00 mchana mkutano unafanyika mtera
chamwino saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano unafanyika chilonwa
20/10/2015 ruvuma songea saa 3:30 hadi 5:00 mkutano unafanyika songea mjini
iringa iringa mjini saa 6.30. Hadi 8.00 mchana mkutano unafanyika iringa mjini
dodoma dodoma mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika dodoma mjini
21/10/2015 shinyanga kahama saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano unafanyika kahama mjini
shinyanga mjini saa 6.00 hadi 8.00 mchana mkutano unafanyika shinyanga mjini
mwanza jiji la mwanza saa 10.00.hadi 12.00 jioni mkutano unafanyika nyamagana
22/10/2015 arusha jiji la arusha saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika arusha mjini
kilimanjaro moshi mjini saa 6.00 hadi 8.00 mchana mkutano utafanyika moshi mjini
tanga tanga mjini saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika tanga mjini
23/10/2015 dar es salaam temeke saa 3:00 hadi 4.30 asubuhi mkutano unafanyika mbagala
ilala saa 5:30 hadi 7:00 mchana mkutano unafanyika wilaya ya ilala
kinondoni mkutano utafanyika jimbo la ubungo
24/10/2015 dar es salaam wilaya zote saa 1.00 asubuhi hadi 12.00 jioni mkutano unafanyika jangwani.


Mchakamchaka huo ni mbio ndefu. Mungu muweza wa yote na awe nasi wakati wote. Amen. 
25/10/2015 Siku ya kupiga kura kwa Rais Lowasa, Mbunge UKAWA, Diwani UKAWA.

Maelfu ya Wakazi wa Dar es salaam wamsindikiza Edward Lowassa leo kwenda Kuchukua Fomu NEC


 
Wananchi wakimsindikiza Waziri mkuu msaafu Edwald Lowassa (CHADEMA) wakati akielekea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Demokrasioa na Maendeleo (CHADEMAwakitokea ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam leo.