Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Msafara wa Mheshimiwa Sugu wavamiwa jijini Mbeya

Gari la Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu likiwa kituo cha Polisi kati jijini Mbeya mara baada ya kushambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM
Sugu akiwa kituo cha Polisi na wafuasi wake.Picha Kenneth Ngelesi Mbeya .


MGOMBEA ubunge  kupitia chadema jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi leo  amejikuta katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na mawe na wafuasi wanaosadikiwa kuwa ni wa chama   cha mapinduzi CCM na kwamba katika tukio hilo watu wawili wamejeruhiwa akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha mgombea huyo 

Tukio hilo la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea majira ya saa 11 za jioni katika eneo  la barabarani lililopo katika Kata ya Ghana mtaa wa Mbata jijini hapa  ambapo inasemekana mgombea huyo alikuwa  katika harakati za kampeni kuomba kura kwa wananchi wa Iziwa  ambapo mgombea huyo alikuwa ndani ya gari yake yenye namba za usajili T161 CPP Toyota  Land Cruser VX .

Awali, wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM, walikuwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wao ngazi ya Udiwani katika kata ya Ghana iliyopo ndani ya Jiji la Mbeya, hivyo wakiwa kwenye harakati hizo inasemekana walishangaa kuona msafara wa sugu ukipita katikati ya mkutano huo hivyo kushindwa kuvumilia na kuanza kurusha mawe huku wengine wakishikana mithili ya kutaka kupigana.

Katika vurugu hizo gari aliyokuwa amepanda mgombea huyo  lilipasuliwa kioo cha mbele na gari ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mbeya, ikipasuliwa kioo cha mbele .
Aidha Vurugu hizo zimesababisha   majeruhi wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya akiwemo dereva wa mbunge huyo na mfuasi mmoja wa chadema.

Kutokana na hali hiyo  mgombea huyo wa ubunge mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema alilazimika kuikatisha zoezi lake la kuongea na wakazi wa Kata ya Iziwa iliyopo Jijini Mbeya kwa muda, kutokana na kulazimika kuripoti katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.

Mgombea huyo ilimlazimu kufika kituoni na kuchukuliwa maelezo na baada ya hapo aliruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kisiasa lakini gari yake yenye namba za usajili T161 CPP aliyokuwa akiitumia katika kampeni zake ikibaki polisi.

Hata hivyo, mgombea huyo alipomaliza kutoa maelezo  katika kituo cha polisi cha kati cha Wilaya ya Mbeya, aligoma kuzungumza na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa kwenye eneo la tukio na kuwataka wafike katika mkutano kwani ndipo atakapotolea ufafanuzi wa suala hilo hilo

Chanzo: JAMIIMOJABLOG MBEYA 

Juma Haji Duni aliteka jimbo la Busanda mkoani Geita

 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
umati wa watu.

Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwasili katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita leo. (Picha na Francis Dande)
 Msafara wa mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni ukiwasili katika kata ya Katolo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwapungia mkono wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa uliofanyika katika kata ya Katolo jimbo la  Busanda mkoani Geita.
 Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwapungia mkono wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa uliofanyika katika kata ya Katolo jimbo la  Busanda mkoani Geita.

Breaking News:Waziri Mkuu Mstaafu FREDERICK SUMAYE ahama CCM na Kuhamia UKAWA

Waziri Mkuu Mstaafu, Ndugu Frederick Sumaye hatimaye leo ametangaza Rasmi kukihama chama chake cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Umoja wa Katiba ya Wannanchi  (UKAWA) japokuwa Sumaye hakuweka wazi ni Chama gani ataingia.
Sumaye ameitoa Kauli yake Leo kwenye Hoteli ya Ledger Plaza,Kunduchi jijini Dar Es Salaam katika Mkutano na Waandishi wa Habari ulioandaliwa na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
 Mbali na kutangaza kukihama CCM, Mheshimiwa SUMAYE alielezea Mapungufu kibao ya CCM katika Mchakato wa kumtafuta Mgombea wa Urais kupitia CCM.
Pia Ndugu Sumaye alikosoa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulhaman Kinana nchi nzima kwa kuikosoa Serikali wakati ndiyo Chama kilichoiunda Serikali. Sumaye alisema,
"Ziara ya Katibu Mkuu ilikuwa ni kuipaka Matope Serikali na si kukijenga chama".
Ndugu Sumaye pia alieleza kuwa CCM imepoteza uelekeo na kusema kuwa hata chama kifanye jambo lipi lakini ifikie hatua lazima watu watakichoka.
Na amehaidi kumsaidia Lowassa kufanikisha Malengo aliyoyataka kuyafanya kama angeteuliwa kuwa Mgombea wa Urais kupitia CCM.