Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange.
HUENDA ikawa kweli Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange amenasa ujauzito unaosemekana kuwa ni wa staa wa muziki kutoka Naija, Davido baada ya kuweka picha tata mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masogange aliweka picha ya Davido na kuandika ‘I’m missing him’ na baada ya sekunde kadhaa tena akaweka picha nyingine ilioonesha majibu ya ujauzito kuwa amenasa.
Hata hivyo baada ya kuandamwa na mashabiki alizifuta zote hali iliowafanya mashabiki wawe njia panda.Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu katika sherehe ya kuzaliwa ya Davido.
Kama kweli Masogange atakuwa na ujauzito kama inavyosemakana na ikajulikana ni wa Davido basi Davido atakuwa na mtoto wa pili baada ya wa kwanza aliyenaye ambaye amezaa na Sophie Momodu wa Nigeria.
;