Showing posts with label Davido. Show all posts
Showing posts with label Davido. Show all posts
Je!Masogange kumzalia Davido?

Je!Masogange kumzalia Davido?

f6f8b2de90c711e3816c12045ea5e329_8
Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange.
HUENDA ikawa kweli Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange amenasa ujauzito unaosemekana kuwa ni wa staa wa muziki kutoka Naija, Davido baada ya kuweka picha tata mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masogange aliweka picha ya Davido na kuandika ‘I’m missing him’ na baada ya sekunde kadhaa tena akaweka picha nyingine ilioonesha majibu ya ujauzito kuwa amenasa.
davido
Hata hivyo baada ya kuandamwa na mashabiki alizifuta zote hali iliowafanya mashabiki wawe njia panda.Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu katika sherehe ya kuzaliwa ya Davido.


Kama kweli Masogange atakuwa na ujauzito kama inavyosemakana na ikajulikana ni wa Davido basi Davido atakuwa na mtoto wa pili baada ya wa kwanza aliyenaye ambaye amezaa na Sophie Momodu wa Nigeria.

Davido atangaza kufanya Collabo na Joh Makini


Hakuna surprise nzuri kama ile ambayo hukuwahi kuona hata dalili, na kwenye muziki hasa kwa msanii wa Bongo hakuna kitu kizuri kama msanii mkubwa wa nje kuanza kutease ujio wa kazi yenu hata kabla yako. Ndicho kilichotokea usiku wa Sept 18 pale staa wa Nigeria, Davido alipotweet kuwa kuna collabo yake na Joh Makini inakuja. Bado haijajulikana kama ni wimbo wa Davido kamshirikisha Joh Makini au Joh kamshirikisha Davido au ni wa wote. 
Hii ni hatua nyingine kubwa ya safari ya Joh Makini kwenda kimataifa, baada ya kufanya collabo na AKA na kuwa kwenye matayarisho ya kufanya collabo nyingine na rapper KO wa Afrika Kusini, mashabiki wa rapper huyo wa Weusi watarajie collabo hiyo ya Davido na Mwamba wa Kaskazini.