Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts
Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts

Diamond Platnumz na Zari ndani ya mahaba mazito Sweden

 
Watakufanya utamani kupenda ukapendwa – maake kunakupenda usipendwe na badala yake ikawa tu karaha, mapenzi usiyafurahie tena. Lakini kwa Zari the Bosslady na Diamond Platnumz ni mahaba mazito kama ya Romeo and Juliet kwenye visa vya William Shakespeare. Wenyewe wanajiita Mr and Mrs Smith aka Brad Pitt na Angelina Jolie.
Mapenzi yao (ambayo walau yanadhihirika kwa picha zao za Instagram), yanaweza kuwapa wivu uliochanganyikana na hasira maex wao. Jioneee mwenyewe picha zao wakiwa backstage kabla ya hitmaker huyo wa ‘Make Me Sing’ hajapanda stejini huko Stockholm, Sweden. 


Bifu la Diamond Platnumz na Ali Kiba Lazua Haya

Ni ukweli kuwa Diamond na Alikiba ni wasanii ambao hawapatani kwa muda mrefu.
Kutokana na ugomvi wao uliopo umepelekea mpaka mashabiki wao kuanzisha team, team hizi zinakuwa zinamsupport msanii wao na kumpinga mpinzani wao.

Diamond aliwahi kuhojiwa kwenye kipindi cha Sporah Show alisema, “Kuna wimbo wa Alikiba ‘Singel Boy’ nilimuomba Alikiba kuingiza sauti tulipokuwa studio alikataa na kusema kuwa nataka mteremko.”

Alikiba aliwahi kusema, “Kwenye wimbo wa ‘Lala Salama’ niliingiza sauti yangu lakini nilishangaa kuona sauti yangu imefutwa kwenye wimbo huo, kibaya zaidi ametumia melody yangu niliyorekodia mwanzo.”

Hakuna mwenye uhakika wa hili kuwa nani ni mkweli na nani anatudanganya. Ugomvi wao unazidi kuwa mkubwa kila siku, sasa hivi umeenda mbali zaidi mpaka msanii atakayekuwa karibu na mmoja kati ya hawa wawili wenye ugomvi mwingine anakuwa anachukia.

Ukiwa karibu na msanii mmoja unakosa support ya upande wa pili, hata kama umeingia kwenye mashindano hutaweza kupigiwa kura na mashabiki wa team nyingine. Hili linarudisha nyuma muziki wetu Angalia kilichotokea kwa Ommy Dimpoz hutataka kuangalia tena nyuma, unakumbuka Wema Sepetu mwanzo alikuwa team gani na sasa yuko wapi? Vipi Jokate kilichomtokea kwenye pande zote mbili kwa sasa unadhani atakuwa wapi tena?

Angalia support wanayopeana Wanigeria kwenye tuzo na muziki wao, hawaonyeshi tofauti zao japo wapo wengi hawapatani. Kwanini tugombee fito wakati tunajenga nyumba moja? Ni ukweli usihitaji ushahidi, Diamond akiingia kwenye tuzo zozote mashabiki wa Alikiba hawampigii kura wanaona ni bora kumpigia kura msanii wa nje ili Diamond akose hiyo tuzo.

Hilo pia lipo kwa upande wa pili kama Alikiba akiingia kwenye mashabiki wa Diamond hawampigii kura. Hata kama Wizkid ana ugomvi na Davido mashabiki wao hawawezi kumpigia kura Diamond au Alikiba ili ashinde tuzo.

Kuna haja wa kuweka tofauti pembeni na kuhakikisha muziki wetu unafika mbali zaidi, ‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, unajisikiaje tunaposhiriki kwenye tuzo za nje kwenye category moja unawaona wapo wasanii wanne kutoka Nigeria na mmoja tu ndiyo wa Tanzania.

Utajisikiaje siku ukiona Jay Z akapenda kufanya kazi na msanii wa Tanzania? Kwa hili lililopo sasa hivi kufika huko ni mbali sana, kila team inafanya msanii mwingine asifanikiwa. ‘Adui muombee njaa’, kwetu imekuwa tofauti tunaombeana wenyewe hiyo njaa.
Diamond azungumzia collabo mpya na Yemi Alade na jinsi Zari alivyobadilisha maisha yake

Diamond azungumzia collabo mpya na Yemi Alade na jinsi Zari alivyobadilisha maisha yake

12558876_229434130733454_1488760884_n

Diamond Platnumz na Yemi Alade wanatarajia kuja na collabo mpya.Taarifa hiyo imetolewa na muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ alipokuwa akiongea na na D’Mike wa kipindi cha Mseto cha Radio Citizen. Amesema yeye na Yemi tangu wakutane kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, wameendelea kuwa washkaji wa karibu.
“Wiki mbili zilizopita amenitumia nyimbo yake mpya ambayo tutafanya, na ukiisikiliza hiyo nyimbo ina mahadhi ya kinyumbani East Africa kabisa, siwezi kusema jina inaitwaje japokuwa jina pia ni la Kiswahili,” alisema Diamond.
Katika hatua nyingine, Diamond alieleza jinsi ambavyo Zari amebadilisha maisha yake.
“Kwenye siku hii nzuri maalum ya Valentine’s kitu kikubwa nitakachoweza kumwambia [Zari] ni kwamba nampenda sana na kiukweli amecheza part kubwa sana katika maisha yangu mpaka hapa nilipo,” amesema.
“Amenizalia mtoto ambaye nilikuwa na ndoto hiyo siku zote na kila siku amekuwa akinifanya napevuka kwasababu nakuwa na akili za kimaisha natoka katika utoto nakuwa katika utu uzima ambao unanifanya niweze kutengeneza hata misingi mizuri ya kazi yangu pia. Ukisikiliza nyimbo zangu, strategy zangu za kimuziki zinazidi kupevuka. Ananitunzia moyo wangu vizuri sababu nina mapenzi naye mazito.”
UMBEYA:Diamond, mama’ke kikao kizito!

UMBEYA:Diamond, mama’ke kikao kizito!


diamond-platnumzSupastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mama’ke mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ wamelazimika kukaa kikao kizito ili kupata muafaka wa mzazi mwenzake na staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurejea Bongo na kuishi katika nyumba moja na mkwewe huyo ambaye walipishana kauli hivi karibuni.
mama-diamondMama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’.
Hivi karibuni, Zari aliyekuwa akiishi na mama Diamond nyumbani kwake, Tegeta-Madale jijini Dar, walipishana kauli na mzazi huyo sambamba na ndugu zake hadi kufikia hatua mrembo huyo aliyezaa mtoto mmoja na Diamond (Tiffah) kurejea nyumbani kwake Afrika Kusini kupisha kile alichokiita ni ‘uswahili’.
zari3Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Chanzo makini kimeeleza kuwa, baada ya kuona Diamond anampenda Zari na mapenzi yao ni motomoto, familia haikuwa na jinsi zaidi ya kukaa kikao kulijadili kwa kirefu suala hilo na kupata muafaka ambapo habari njema ni kwamba, mama Tiffah anatarajia kutua Bongo siku chache zijazo.
“Diamond si unajua ndiyo kichwa katika familia. Amewaita ndugu akawaeleza dhamira na mikakati yake na Zari hivyo wamekubaliana arejee Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo, hakutaka kufunguka kwa undani akidai ni mambo ya kifamilia.

“Kila kitu kipo sawa. Zari ataibuka na maisha yataendelea kama kawaida, haya mambo ya kifamilia bwana,” alisema Diamond.
Kabla ya kufikia muafaka huo, Zari aliripotiwa kuwa anakuja nchini Desemba 8, mwaka huu wakati mama Diamond akionekana kupinga lakini hatimaye muafaka umepatikana.

Diamond Platnumz:Sitaki Kabisa Kushika Simu ya Zari Naogopa kuumia!

Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Zari ni watu ambao huwa hawapendi kupekuliana simu simu zao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kusababishwa na simu za mikononi. Simu za mikononi huwa ni moja ya chanzo cha ugomvi kwa wapenzi wengi, na tumekuwa tukisikia story za couple nyingi kuingia kwenye matatizo kutokana tu na mmoja kukuta ujumbe au picha zenye utata kwenye simu ya mwenzie hata kama haimaanishi kuwa anamsaliti.
 Diamond na Zari wote ni watu maarufu ambao wana mashabiki wa jinsia tofauti, hivyo kwa kutambua mazingira ya kazi zao wameona ni bora kuaminiana bila kupekuana kwenye simu zao. “Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa,” alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari. Diamond aliendelea kutoa sababu za kutoshika simu yake, “sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye (Zari) ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi sometimes anaweza akamjibu mtu akaitikia tu poa, kwangu mimi kikanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo ikaniumiza, kwahiyo sitaki kabisa kushika simu yake.” Pamoja na kwamba yeye hashiki simu ya mpenzi wake, vipi kuhusu Zari kushika simu yake? “ Simu yangu mi haina password naiachaga tu lakini nafikiri na yeye ni mtu wa dizain hizo ambaye hataki kabisa kudiriki kushika simu yangu, yaani simu zinaleta ugombanishi sana.” 
Diamond pia aliwashauri watu wengine kutoshika simu za wapenzi wao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika. “Kwahiyo simshauri mtu kushika simu ya mpenzi wake, cha muhimu tu kuzingatia kama anakupenda anakujali anakuheshimu na umuone na hivyo vitu, lakini kwenye simu yake mwache afanye chochote anachojua yeye.” Alisema 

Diamond Platnumz wins MTV EMA 2015 Best African Act award

MTV Base today revealed that Diamond Platnumz is the winner of the 2015 MTV EMAs Best African Act. Scores of music fans visited mtvema.com to vote for Diamond Platnumz, who beat incredible competition from AKA, Yemi Alade, Davido, and DJ Arafat. Diamond Platnumz will now go up against the winning act from India to be named Best Africa/India Act ...
Pedeshee katunzi ataka DNA ya Tiffah wa Diamond Platnumz!

Pedeshee katunzi ataka DNA ya Tiffah wa Diamond Platnumz!

toto d
MAKUBWA tena! Wakati Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akijinasibu kuwa mtoto Latiffa ‘Tiffah’ ni damu yake, pedeshee maarufu Bongo, Muzamil Katunzi ameibuka na kumtaka staa huyo wa Bongo Fleva kupima kipimo cha vinasaba (DNA) ili kujiridhisha kama kweli ni damu yake, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
tiffahMtoto Latiffa ‘Tiffah’
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo, pedeshee Katunzi amekuwa akitajwatajwa kuwa huenda mtoto huyo ambaye Diamond anajinasibu kuzaa na mfanyabishara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’  ni wake, kwani Katunzi aliwahi kuwa na ukaribu na mwanamke huyo.
“Watu wanamtajataja sana Katunzi katika hili suala, hivyo huenda kuna ukweli maana si mnakumbuka Zari na Katunzi waliwahi kuwa klozi?
TIFFAH DIAMOND (2)Diamond, Zari na mtoto Latiffa ‘Tiffah’
ETI SURA NI KATUNZI MTUPU
“Mtafuteni Katunzi mumbane vizuri maana watu kibao wanasema sura ya Tiffah ni yeye mtupu, sasa hapa na hata picha zinazotambaa kwenye mitandao, wameunganisha picha ya Katunzi na Tiffah yaani damdam,” kilimwaga ‘ubuyu’ chanzo hicho.
ZARIKatunzi na Zari
KATUNZI ANASEMAJE?
Waandishi wetu baada ya kupenyezewa ubuyu huo, walilazimika kufunga safari hadi Mikocheni jijini Dar kwenye ofisi za pedeshee Katunzi kutaka kujua kama madai hayo ni ya kweli au la!
HUYU HAPA KATUNZI
“Kusema kweli mimi nilifahamiana na Zari kabla ya Diamond, ila ukaribu wetu uliisha pale tu niliposikia Zari anatoka na mdogo wangu Diamond, sasa sijui watu wanasema ninafanana na Tiffah kwa kigezo kipi, ila nadhani watu wamekuwa na hisia mbaya tu maana sina uhakika kama Zari anaweza kuwa na mtoto wangu na asiniambie maana hatukuwahi kukosana hata siku moja.
AMTAKA DIAMOND APIME DNA
“Kutokana na hili, ningependa tu kumshauri Diamond kama hatajali sana aende kupima DNA ili awe na uhakika na haya yanayozungumzwa maana bila kufanya hivi sidhani kama atakuwa kweli na amani moyoni mwake, kwani maneno siku zote huumba jambo, yawezekana kabisa Tiffah hana uhusiano na mimi lakini akafananishwa tu kwa kuwa kuna watu walikuwa wanafahamu juu ya uhusiano wangu na Zari,” alisema Katunzi.
DIAMOND SASA
Mapaparazi wetu baada ya kusikia maneno ya Katunzi, walimtafuta Diamond ambaye alisema yeye ataendelea kusimamia msimamo wake kwamba Tiffah ni damu yake na anashangaa jinsi maneno yanavyoibuka kila siku kuhusu mtoto wake.
“Mimi sioni sababu ya kujibizana na mtu juu ya Tiffah kwani kila mtu anaongea anavyojisikia,  na wengi wao wanatafuta niwajibu ili waweze kufanikisha azma yao, wananishangaza sana watu wa aina hii kila siku kuibuka na jambo,” alisema Diamond.

Chanzo: Global Publisher

Five Things that You didn't Know about Diamond Platnumz's daughter

Five Things that You didn't Know about Diamond Platnumz's daughter


1.She is the Daughter of Singers! Diamond is a singer as well as her mother Zari
2.She has famous Parents as well as she is right now
3.She is the youngest rich in Tanzania since up to this moment she has only 3 days but she has 50mil in Bank the money many people die without touching it
4.She is very popular than many super stars in Tanzania since up to this moment she has 63.1k
Instagram followers
5.She is paid monthly 1 mil as a salary of being The BabyShop Brand Ambassador at
@Msasani_city_mall & @pugu_mall


Message from Zari 'the bigboss Lady' to her Kipenzi Diamond Platnumz to wish him Happy Birthday

Message from Zari 'the bigboss Lady' to her Kipenzi Diamond Platnumz to wish him Happy Birthday

Today is superstar Diamond Platnumz' birthday, his baby mama Zari The Boss lady took to social media by writing then below heart-felt message...

" Everything i could say has been said and you've prolly heard it over and over but; this year you celebrate your birthday as a father a blessing and a gift that's bigger than life its self. Your birthday gift came earlier this year there isnt anything else i can give you. So allow me to wish you a happy birthday as BABA TEE. May the almighty God continue showering you with blessings over your career and MOST IMPORTANTLY to grant you many more years to see @princess_tiffah start her grade one, see her to university, date boys (i know you don't wana hear this but its going to happen 😂), hand her out in marriage and lastly to be able to see our grand kids (Tiffah's babies) that said, Allow me to wish you a happy birthday my kipenzi 😍 @diamondplatnumz"