Showing posts with label Kidoa. Show all posts
Showing posts with label Kidoa. Show all posts

Udaku:Masogange kumharibu Kidoa

 Agnes Gerald  Masogange
Video Queen nyota, Agnes Gerald maarufu kama Masogange anadaiwa kutaka kumharibu muuza nyago chipukizi Asha Salum ‘Kidoa’ baada ya wadau kutilia shaka ukaribu wao.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, katika siku za hivi karibuni mabinti hao wamekuwa na urafiki wa karibu, wakichati mambo mengi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kitu kinachoonesha huenda ushosti wao ukafika mbali zaidi ya hapo. “Si unajua Masogange ana zile dili zake za kwenda mara kwa mara Sauz huku ikiwa haijulikani hasa anafuata nini? Na si unakumbuka ule msala wake wa kukamatwa na madawa ya kulevya? Sasa wadau wanahofu asije naye akaingizwa kwenye mchongo,” kilisema chanzo hicho.
Asha Salum ‘Kidoa’
Katika kuweka sawa madai hayo, gazeti hili liliwasiliana na Kidoa ambaye alifunguka; “Mimi ni mtu mzima na akili zangu timamu, siyo kila rafiki utakayekuwa naye basi lazima uige tabia zake, halafu Masogange siyo rafiki yangu kihivyo, kawaida tu!”
Kwa upande wake, Masogange alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kwa kifupi; “Ulishawahi kuniona nikienda naye Sauz, au ulishawahi kuniona naye kwenye ndege, kifupi mimi sinaga rafiki.”

Umbea:Kidoa, Farid Uwezo wabambwa kimalovee

Video Queen mwenye mvuto wa aina yake, Asha Salumu ‘Kidoa’
KABANG! Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Asha Salum ‘Kidoa’ na msanii wa sinema za Kibongo, Farid Uwezo wamebambwa live wakiwa kimalovee kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar.

Wawili hao walikuwa wakilishana matunda aina ya strawberry, walipoulizwa kulikoni walidai ni marafi kitu hakuna kinachoendelea kati yao.
fariduwezoMsanii wa sinema za Kibongo, Farid Uwezo.
Mahaba Niuwe:Kigogo atenga Milioni 10 kumnasa Kidoa

Mahaba Niuwe:Kigogo atenga Milioni 10 kumnasa Kidoa

Video Queen mwenye mvuto wa aina yake, Asha Salumu ‘Kidoa’.
FEDHA inaongea! Kigogo mmoja aliyeomba jina lake lihifadhiwe, amedaiwa ‘kukolea’ kimahaba kwa Video Queen mwenye mvuto wa aina yake, Asha Salumu ‘Kidoa’ kiasi cha kutangaza dau la shilingi milioni kumi.
Chanzo chetu makini kilicho beneti na kigogo huyo anayemiliki yadi kadhaa za magari hapa Bongo, kimesema bosi huyo kila wakati amekuwa akimzungumzia Kidoa na kuahidi kumpa shilingi milioni kumi endapo tu atafanikiwa kulipata penzi lake.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi na kusema kwamba kigogo huyo amekuwa akihaha kila kona kutafuta namba za simu za Kidoa ili aweze kuzungumza naye na kuelewana na hatimaye kumpa malavidavi.

“Jamaa yangu amechanganyikiwa mno, hatulii, kila wakati anamuulizia Kidoa huku akiahidi kumpatia milioni kumi kama tu atafanikiwa japo kuwa naye usiku kucha kwani kama mademu kaona wengi, ila kwa Kidoa, moyo wake umegota kabisa. Kila siku anahaha kutafuta namba yake, hajaipata ila yupo radhi kuinunua kwa gharama yoyote ile,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya kigogo huyo ambapo alikiri kumsaka mrembo huyo kwa hali na mali lakini akaomba asiandikwe gazetini.
“Jamani kama mnaweza mnisaidie. Mtoto kaumbika, nilianza kumuona kwenye ile video ya Akadumba ya Nay wa Mitego sasa picha zake zinazotoka katika magazeti zinanidatisha kweli nisaidieni ila ‘please’ msiniandike gazetini,” alisema kigogo huyo.