Magari na Ofisi Kuwa "Guest" Bubu..... Ni Fedheha.


Habari za leo wadau wa Blog hii?

Kwa takriban miezi 6 nimekuwa busy na majukumu mengine ya kitaifa kiasi cha kukipa mgongo kijiwe chetu hali inayopelekea kushindwa kupeana habari na mafunzo mbali mbali kwa mustakabali wa Ndoa zetu.

Kwa leo nienze na samahan kwa ukimya wangu, halafu nijikite katika kichwa cha mada yetu leo. Katika jamii yetu ya leo, suala hili limekuwa likishika usukani kila leo, waanyakazi wa kada mbali mbali bila kujali nyadhifa zao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao na kugeuza ofisi zao kuwa Machaka ya kufanyia madudu yao.

Hili limeenda mbali kiasi cha kupelekea kugeuza magari kuwa Guest Bubu, hili halipendezi na sio wafanyakazi peke yao bali hata wafanya biashara. Hili halivumiliki na wahusika wajitahidi kuepukana nayo usije ukijikuta unapata matatizo na wako wa ukweli sababu a kulazimisha starehe ya muda mfupi na huyo mchepuko wa ghafla.

Weekend njema wadau wangu,......Tumerudi Upyaaaa.