Takukuru Imewapandisha Kortini Wabunge watatu wanaotuhumiwa kwa rushwa

 
Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu hivi punde kwa tuhuma za rushwa.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa toka kwa Taasisi za Kiserikali ili kuweza kusaidia taarifa zao ambazo zinamapungufu zipitishwe bila kupingwa 

Wananchi wagombea kiti alichokalia Rais Magufuli Jijini Mwanza


Mgahawa aliotumia Rais John Magufuli kupata mlo wa mchana na msafara wake juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza, umekuwa kivutio kwa wateja wengi wakinunua chakula na kutaka kukalia kiti na meza alivyotumia kiongozi huyo.
Meneja wa mghahawa huo wa Victoria, Elizabeth Maneno (pichani) alisema jana kwamba hali hiyo ilijitokeza mara baada ya Rais kuondoka hapo.
“Hata leo tumepokea wateja wengi kulinganisha na siku nyingine, baadhi yao wanaagiza chakula kwa sharti la kutaka kukikalia kiti na meza aliyotumia Rais Magufuli,” alisema Elizabeth.

Akizungumzia hali ilivyokuwa juzi kabla na wakati wa ugeni huo meneja huyo alisema:“Ilikuwa ni hofu na woga uliochanganyika na furaha kumwona Rais akiingia kwenye mgahawa wetu wa chai ya rangi ya Sh200 na ya maziwa Sh300.

“Mshtuko wetu uligeuka furaha baada ya kubaini kuwa oda ya sahani 28 za kubeba (takeaway), tulizoagizwa mapema asubuhi bila kuelezwa zinakoenda zilikuwa za ujumbe wa Rais,” alisema na kuongeza:

“Kabla Rais Magufuli hajaingia kwenye mgahawa wetu, alikuja mtu mmoja tusiyemfahamu na kuagiza sahani 28 za chakula kwa gharama ya Sh5,000 kila moja,”

Alisema baada ya kumtaarifu mteja wake kuwa chakula kiko tayari, alielekezwa kuandaa meza na viti kwa sababu wageni wake (wa mteja), sasa wameamua kula palepale mgahawani.

“Ghafla tulimwona Rais anaingia ndani ya mghahawa wetu; kwanza tulishikwa hofu, woga na kihoro tusijue tufanye nini hadi tulipogutushwa na aliyetoa oda kwa kutuagiza tugawe chakula alichoagiza,” alisema meneja huyo; “hapo ndipo tulipobaini kumbe chakula kile kilikuwa cha ugeni wa Rais.”


Pamoja na chai ya rangi na ya maziwa, mghahawa huo pia unauza vyakula vya aina mbalimbali kwa bei kati ya Sh1,500 hadi Sh5,000 kwa vyakula vya kubeba, huku soda ikiuzwa kwa Sh500 kwa chupa

Gerald Hando, Paul James waondoka Clouds FM

Gerald Hando na Paul James, wanadaiwa kuachana na Clouds FM, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
Wawili hao wamekuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha kituo hicho kwa miaka mingi.
Gazeti la Mwananchi limedai kuwa watangazaji hao wamemaliza mkataba na kituo hicho na hakijapenda kuwaongezea

Nafasi za Kazi kutoka Serikalini


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF HEALTH, COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER, ELDERLY AND CHILDREN
PRIVATE HEALTH LABORATORIES BOARD
EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
Private Health Laboratories Board (PHLB), is the Government Institution under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children which registers and manages all Private Health Laboratories in Tanzania (Mainland), Vacancies exist at the Board`s Head Office in Dar es Salaam and applications from suitably qualified and competent persons are invited to fill the following posts:-
1.    Laboratory Quality Assurance Officer (1 post)
Duties and Responsibilities
•    To implement activities involved in Laboratory Quality Assurance Framework, Laboratory Standard Guidelines, training curriculum and modules so that they meet International standards requirements.
•    To monitor quality of health Laboratory Services in supporting the provison of essential intervention health packages in the private laboratories.
•    To work towards Accrediting health laboratory through intenetionally recognized accrediting board.
•    To document all laboratory quality activities including submission of reports to relevant authority.
•    To liaise with national laboratory quakutt ststens coordinator on all matters conceming private health laboratories quality systems.
•    To monitor all EQA results and provide feedback on the effectiveness and performance of private health laboratories nationwide.
•    To perform competence assessment to laboratory staff.
•    To perform any other relevant duties as may be assigned from time to time by Registrar.
Qualifications and Experience
•    Medical laboratory technologist or medical laboratory scientist from recognised institutions and registered by health laboratory practitioners council.
•    Working experience of three years implementing quality management system (QMS) the quality assurance officer will report direct to the Registar-Private Health Laboratory Board.
===========
2.    Medical Health Laboratory Authorized Inspector (1 post)
Responsibilities
•    To monitor all private health laboratories in Tanzania Mainland.
•    To inspect health laboratories, health Laboratory products and supplies countrywide.
•    To prosecute offenders by taking in implementing the Act 10 of 1997 and laboratory regulations at national.
•    To coordinato preparation of samples for quality assessment, analyze results and disseminate the report.
•    To perform any other duties assigned by the registrar from time to time.
Qualifications and Experience
•    Medical Laboratory Technologist or Medical Laboratory scientist registered by health laboratory practitioners council
•    Working experience of three years.
As a medical laboratory authorized inspector she/he will report to the Registrar – Private Health Laboratories Board.
How to Apply
Interested and qualified individuals should submit their applications enclosing detailed CV`s two passport-size photographs, photocopies of academic and professional certificates. Names and addresses of three referees to the address under mentioned not later than 8th April, 2016. For all posts mentioned above, the employment condition is for two years contract subject to be renewable.
Private Health Laboratories Board is an equal opportunity employer.
Registrar
Private Health Laboratories Board
P.O.BOX 9073
DAR ES SALAAM – TANZANIA

Mrembo Amvamia Dully, akiona cha mtema kuni

Mrembo huyo baada ya kupanda jukwaani ili acheze na Dully.

DAR ES SALAAM: Hii ni aibu ya Pasaka! Mrembo mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, mwishoni mwa wiki alijikuta akifedheheka baada ya kushushwa jukwaani, alikoenda kwa lengo la kucheza pamoja na mkongwe Dully Sykes aliyekuwa akitoa burudani huko Sunrise, Kigamboni jijini Dar.
Akitolewa jukwaani hapo
Akiwa amevaa mavazi yaliyoonesha sehemu kubwa ya mwili wake, huku akionekana kuzidiwa na kiburudisho, mrembo huyo alikuwa akicheza kwa kukata kiuno hovyo kiasi cha kuwa kero kwa mashabiki wengine.
Ilikuwa majira saa 6 usiku baada ya wasanii kuanza kupanda jukwaani. Ishu kamili ilikuja baada ya Msaga Sumu kufungua shoo kisha wasanii wengine kuburudisha, ilipofika zamu ya Dully, mrembo huyo alikurupuka kutoka alikotoka na kupanda jukwaani kumvamia akiwa amevaa nguo zenye rangi iliyofanana na mwili. 

Akishushwa jukwaani mkuku.
Lakini kabla hajafanya lolote, mmoja wa vijana waliokuwa wameongozana na Dully, alimdhibiti mrembo huyo kwa kumshusha jukwaani. Kuonesha kuwa alikuwa ‘crezi’ na mkali huyo wa kibao cha Nyambizi, mrembo huyo aliendelea kucheza kwa furaha huku akishangilia kana kwamba hakukuwa na chochote kilichotokea.
Dully Sykes
Baadhi ya wasanii wakongwe waliokuwepo katika tamasha hilo lililoandaliwa na Promota Majid Bonga, baada ya kutimiza miaka 25 kama mdau wa sanaa ni pamoja na Juma Nature, Sister P, Manzese Crew, Zig Zag Crew, Solid Ground Family, Inspector Haroun, Afande Sele, Soggy Doggy, Mabaga Fresh, Dully Sykes, Jaffarai na wengine kibao

Udaku:Masogange kumharibu Kidoa

 Agnes Gerald  Masogange
Video Queen nyota, Agnes Gerald maarufu kama Masogange anadaiwa kutaka kumharibu muuza nyago chipukizi Asha Salum ‘Kidoa’ baada ya wadau kutilia shaka ukaribu wao.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, katika siku za hivi karibuni mabinti hao wamekuwa na urafiki wa karibu, wakichati mambo mengi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kitu kinachoonesha huenda ushosti wao ukafika mbali zaidi ya hapo. “Si unajua Masogange ana zile dili zake za kwenda mara kwa mara Sauz huku ikiwa haijulikani hasa anafuata nini? Na si unakumbuka ule msala wake wa kukamatwa na madawa ya kulevya? Sasa wadau wanahofu asije naye akaingizwa kwenye mchongo,” kilisema chanzo hicho.
Asha Salum ‘Kidoa’
Katika kuweka sawa madai hayo, gazeti hili liliwasiliana na Kidoa ambaye alifunguka; “Mimi ni mtu mzima na akili zangu timamu, siyo kila rafiki utakayekuwa naye basi lazima uige tabia zake, halafu Masogange siyo rafiki yangu kihivyo, kawaida tu!”
Kwa upande wake, Masogange alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kwa kifupi; “Ulishawahi kuniona nikienda naye Sauz, au ulishawahi kuniona naye kwenye ndege, kifupi mimi sinaga rafiki.”

Dondoo:Zifahamu nchi 10 za Afrika zenye wanawake warembo,Tanzania ikiwemo

 post-feature-image 
Afrika ni bara zuri ambalo limejaa tamaduni mbali mbali, Lugha na watu wa kila aina. Kama ilivyo kila kitu kinakuzidiana, Hivyo katika nchi zilizomo ndani ya bara la Afrika kuna nchi ambazo zinaongoza kuwa na wanawake wenye mvuto. Tunavyo ongelea 'Wazuri/Warembo' hapa ndipo mchanganyano unapo tokea maana ni neno kubwa sana na zito.
Kila moja huona uzuri kwa tofauti yake, Lakini kwa ujumla hatuangalii sura, umbo bali tabia, kujitunza na ushawishi wa kutumia muonekano wako.

NOTE: Mtazamo huu wa Top 10 nchi za Afrika zenye warembo ni kutokana na maoni mengi kutoka kwa watu kwa mujibu wa Afrojuju.net, Hivyo na wewe unaweza kuaj na Top 10 yako yenye nchi ambayo unahizi inawarembo wakali hapa Afrika
10: TANZANIA.
Wanawake wa nchi hii wanasifika kwa uzuri, kutunza nyumba na ujuzi kwenye kitanda. Kama unatafuta mwanamke wa kumpeleka nyumbani kumtambulisha ambaye anajua kutunza nyumba, Basi Tanzania ndipo eneo sahihi.
09: KENYA.
Wasichana wa Kenya niwazuri na wanamahaba, Kama unatafuta msichana ambaye ni mzuri, mwenye mahaba, na anaye jisimamia 'Independent', Mchapa kazi na sio mvivu... Basi kimbilia nchini Kenya.
08: GHANA.
Haitawezekana kukamilisha list ya nchi zenye warembo bila kupitia Gold Cost. Wanasifa ya kuwa Warefu, Wataalamu kitandani, ngozi ya asilia 'Ebony Skin tone' na wana uhalisi wa Muafrika.
07: NIGERIA.
Wanawake wa Nigeria niwazuri kutokana na ukubwa wa maziwa yao na walivyo jengeka miili yao kwa afya. Kati kati ya mwaka wa 1970s na 2011 nchi ya Nigeria imeongezeka kwa idadi ya watu nakusababisha iwe maarufu barani Afrika. Hivyo kama unataka mwanamke ambaye atakuzaliwa watoto wazuri basi Nigeria ndipo ukimbilie.
06: SOUTHAFRICA 'The famous Rainbow Nation'.
Afrika Mashariki ni nyumbani kwa wanawake warembo barani Afrika, kuwanzia Cape Town, Johannesburg, Pretoria na Durban. Wanawake wa Afrika Mashariki utawapata wenye uweupe wa chotara au uweusi halisi wa Afrika.
05: ANGOLA 'Doughters of Atlantic cost'.
Nchi ya Angola unaweza kusema ni kama Brazil ndogo kwa wasichana wazuri na warembo, Wasichana wake wakiwa wana rangi ya chocolate scados. Wasichana wa Angola baazi ni Supermodels ambayo itakuchanganya akili kabisa.
04: CAPEVERDEISLAND.
Sio nchi maarufu barani Afrika wala hata kupata wataa kwenda kuitazama, Lakini kisiwa hicho kidogo ni nyumba ya wasichana na wanawake warembo walioumbwa Afrika. Wanakauli nzuri ya ukarimu ambayo itakufanya usahau njaa wakati hukula chakula.
03: ETHIOPIA 'The cradle of humanity'.
Ustaarabu ndipo ulipo anzia nchini Ethiopia, Wasichana wa nchi hii sio wazuri tu kwa bara la Afrika bali hata ulimwenguni wamekuwa wakisifika kwa uzuri wao unao shawishi kutangaza ndoa. Wengine wamekuwa wakidai uzuri wao umetokana na mchanganyiko wa mbegu 'uzazi' kutoka kwa watu wa Yeamen na Ethiopia wenyewe.
02: SOMALIA 'Vita haiondoi urembo'.
Kama hujawahi kukutana na msichana wa Kisomali basi utakapo kutana naye utachanganyikiwa na kukusababisha uweze hata kusaliti uliye naye. Chukulia mfano wa Iman, Model aliye tikisa ulimwengu kwa mwendo wake wa madaha hadi kila mmoja kushangaa. Wanasifika kuwa na macho mazuri, ngozi ya chocolate, nywele laini na ndefu.
01: RWANDA 'Africa's hidden Apple'.
Niwazuri na wakuvutia, Weusi wa asili, Wana umbo nzuri na ukarimu, Sauti ya kimahaba na urefu wakupagawisha. Wakitembea ni sawa na Twiga nyikani akiwa anatembea. Uzuri wao huwezi kuuelezea.

-Nimekosea? Wewe unadhani nchi gani Afrika ingekuwepo kwenye Top 10 yangu ya leo? Niachie comment hapo chini.

Baada ya kumkwapua Jux…haya ndiyo Maneno ya Vanessa

Mtoto mzuri wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’.
Baada ya kumkwapua Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’ aliyekuwa mpenzi wa modo Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Cliff’ kisha modo huyo kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China, mtoto mzuri wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ameibuka na kumzungumzia ‘mtalaka’ huyo wa Jux.
V-Money alimfungukia modo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum (exclusive) na Global TV Online ambapo pamoja na mambo mengine ya kimuziki, staa huyo anayetamba na Wimbo wa Niroge, alitumia dakika kadhaa kufafanua tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusiana na Jack.
Awali, wanahabari wa Global TV walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu.
“Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini.
Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Cliff’.
Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule gerezani anaposika amekwapuliwa bwana wake (Jux) na pengine haoni kama anamuongezea machungu, Vanessa alifunguka:
“Kwanza kabisa sijamchukulia bwana wake. Namuombea atoke mapema. Ninachoweza kusema, namuombea atoke jela mapema. Matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo anafikiria.
“I don’t think she even think about me at all (sifikirii kama ananifikiria mimi kabisa). Nadhani anawafikiria familia yake na hali ambayo amefungiwa pale. Sidhani kama hata ananiwaza.”
Jack alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guandong Kusini mwa China.
Kutazama mahojiano kamili tembelea www.globaltvtz.com.

Siri mpya Freemason zafichuka!

Jayantilal Keshavji Chande ‘Sir Andy Chande’.
 
Imebainika kuwa, taasisi inaayodaiwa kuwa na imani yenye utata duniani ya Freemason inaanza kupungua nguvu kufuatia wafuasi wake kuachana na nao na kurejea kwenye imani zao za mwanzo chanzo kikiwa kusemwa vibaya kwa taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa memba mmoja wa Freemason jijini Dar, idadi ya wafuasi wa taasisi hiyo inapungua siku hadi siku na sasa, viongozi wake wanahaha kutoa elimu ya kuwafanya waliobaki waendelee kubaki.
TWENDE NAYE HUYU
“Unajua wakati inaanza Taasisi ya Freemason ilipata jina kubwa sana kwani watu wengi maarufu walijiunga, lakini sasa yale manenomaneno kwamba kuna ibada ya kishetani, wanaojiunga wanatoa makafara ndugu zao, mara kuna chakula cha damu, baadhi ya wanachama wakaanza kutoka kurejea kwenye imani zao za awali,” alisema memba huyo
Pete zenye alama ya Freemason.

KUNA IBADA KWELI?
Alipoulizwa kwa nini wafuasi wamekuwa wakiondoka kwa maneno mabaya ya watu kama kweli hakuna ibada,  mwanachama huyo alisema:
“Sifa mbaya, unajua wengine waliona kama wanachafuliwa lakini ukweli wanaujua wao kwamba hakuna ibada za kishetani. Ila tunapokutana wote tunakuwa na maneno ya pamoja kama kuashiria mshikamano wetu.”
TANZANIA KUNA WANACHAMA WANGAPI?
“Kwa Tanzania mpaka sasa kuna wanachama wasiopungua 650. Unajua kikubwa ni masharti ya kujiunga wengi yanawabana, ndiyo maana idadi ni ndogo kwa nchi kama hii yenye watu wasiopungua milioni arobaini.”
NI AKINA NANI?
“Wafuasi wetu wengi wanatoka katika sehemu mbalimbali, kuna walimu, wauguzi, madaktari, watu maarufu, wafanyabiashara wakubwa na wengine ni wanafunzi wa ngazi ya chuo. Lakini tofauti na watu wanavyosema kuwa, kuna viongozi wakubwa wa serikali, si kweli. Viongozi wakubwa wa serikali si wafuasi wetu ila wanaweza kutoa ushauri au kusaidia pale inapobidi.”
KUMBE JENGO LAO LILIKUWA LA BUNGE ZAMANI
Katika mazungumzo hayo, memba huyo alisema kuwa, jengo linalotumiwa kama Ofisi ya Freemason lililopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam, lilikuwa la bunge wakati wa mkoloni na baadaye serikali ya Tanganyika huru, mwaka 1961.
Jengo linalotumiwa na wanachama wa Freemason.
 
UNATAKIWA KUWA MILIONEA ILI KUJIUNGA
Tofauti na watu wanavyodai kwamba, unaweza kujiunga na Freemason ukiwa maskini halafu ukawa tajiri, lakini mwananchama huyo alisema kuwa, anayetaka kuwa mfuasi ni lazima aweze kutoa mchango unaofikia shilingi milioni kuanzia kumi na kuendelea.
KAULI YA SIR ANDY CHANDE YATOA NGUVU
Maneno ya memba huyo yanashibishwa nguvu na aliyewahi kuwa kiongozi wa Freemason ukanda wa Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande ‘Sir Andy Chande’.
Akizungumza wakati fulani jijini Dar es Salaam kwa kuanika hali ya Freemason nchini na duniani kwa ujumla, Sir Chandy alisema kuwa, Tanzania ina wafuasi zaidi ya 600 ambao wanatokana na kada mbalimbali wakiwemo watu maarufu, lakini alisema hakuna viongozi wakuu wa serikali.
HAWATAMBULIKI
Chande alisema kuwa, si kazi rahisi kumtambua mfuasi  wa Freemason lakini wao wenyewe ndiyo wanaofahamiana na kukutana katika vikao mbalimbali ambavyo hufanyika mara moja baada ya siku thelathini.
KUHUSU IDADI KUPUNGUA
Chande alisema kuwa, awali tangu kuanzisha kwake mpaka miaka ya karibuni, wafuasi wa Freemason walifikia 8,000,000 duniani kote lakini kwa sasa wamefikia 6,000,000 kutokana na watu kuielewa vibaya taasisi hiyo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel &Bible Fellowship, Zachary Kakobe.
 
WAFUASI WANATAKIWA KUBAKI NA IMANI ZAO
Sir Andy Chande alikwenda mbele kwa kusema kuwa, ili uwe mwanachama wa Freemason ni lazima mtu huyo aendelee kuwa muumini wa Mungu katika imani yake ya Kikristo au Kiislam.
UMRI NI HUU
Alisema anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi kwa sababu ya uwezo wa kutunza mambo lakini pia akasema ili ujiunge Freemason ni lazima familia ya anayetaka kujiunga ua ndugu zake wajue ili kuepuka matatizo utakapotakiwa kutoa michango.
UWAZI NA SHEHE MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Akizungumza na gazeti hili juzi kuhusu imani hiyo kuwataka wafuasi wake wabaki kwenye imani zao, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum alisema:
“Muumini wa Kiislam, akiwa Freemason ajue si Muislam tena. Wale wana ibada mbaya, haitokani na Mungu tunayemwamini sisi. Wewe Kama ni Muislam halafu ni Freemason jiondoe kwenye Uislam.”
HUYU HAPA ZACHARY KAKOBE
Akizungumza na Uwazi, Jumamosi iliyopita kuhusu imani ya Freemason, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel &Bible Fellowship, Zachary Kakobe alisema:
“Ni unafiki mkubwa kumtumia Mungu aliyeumba mbingu na nchi halafu wakati huohuo ukawa kwenye imani ya Freemason. Chagua moja, Mungu hataki mtu vuguvugu. Kuwa moto au kuwa baridi ijulikane moja. Na wat wajue kwamba, ibada yoyote nje ya Mungu wa kweli ni ushetani.”
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum.
 
KAMANDA SIRO NAYE ASEMA YAKE
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro yeye alisema:
“Freemason ni taasisi ipo kisheria. Ila mimi nataka kushughulika na hao watu mnaowaandika kwamba wanajipatia pesa kwa kuuza fomu feki za Freemason kwa njia ya utapeli. Siku moja nitavaa kiraia halafu nitakwenda pale ofisini kwao nje nikawakamate.”
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ANENA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Yusuf Masauni alipoulizwa juu ya madai kuwa Freemason wanadaiwa kuwa katika imani za kishetani alisema hayo ni madai na hawezi kuyazungumzia kwa sababu hana hakika na hicho kinachodaiwa.

Juma Nature adai mshindani wake kwenye muziki kwa sasa ni Diamond

 Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature amedai msanii pekee ambaye anaweza akashindana naye kwa sasa ni Diamond.
Akizungumza na tovuti ya Times Fm, Juma Nature ameomba wadau kuandaa tamasha ili washindanishwe.
“Watu wanamtukuza sawa lakini watuweke stage moja tuone nani atakamua, unajua tuseme ukweli bongo flava sasa mimi na Diamond ndio wapinzani pekee,” alisema Juma Nature.
Aliongeza, “Watu waandae pambano, na mpunga pia uwepo nioneshe na mimi nguvu yangu ilivyo mtaani,”
Nature amesema anaamini muziki wake aliyokuwa anafanya zamani una nguvu kubwa kuliko huu wa wasanii wa sasa.

Wema Sepetu Atoboa Siri...Aliyekuwa Mume wa Zari Anamtongoza na Ahadi ya Kumuoa

 
Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka kumuoa.
Katika mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu.
“Nilikwenda na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo, wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka nao out pamoja.”
“Mimi nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwishoni ilibidi tuwakubalie lakini kwa masharti ya kuwa wasije wakatuzushia lolote.
“Tulikubali, wakaja, tukakaa nao meza moja, tukabadilishana mawasiliano kama marafiki. Lakini baadaye tukaona wanaongezeka, sikupenda vurugu ya watu wengi, mimi na Ommy tukaamua kuondoka zetu,” alisema Wema.
Akizidi kumwaga siri zake na mwanaume huyo, Wema alisema baada ya yeye kumaliza project yake nchini humo, alirejea Bongo na ndipo Ivan alipozidisha ufundi wa kumuomba urafiki wa kimapenzi huku akimuahidi mambo mengi ya muhimu.
Msikie Wema: “Baada ya hapo tulikuwa tunawasiliana na Ivan, lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, nikaona mwenzangu anaanza kunitongoza, tena akawa anaendelea kila siku licha ya mimi kutomkubalia.”

Aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga.
Wema alizidi kutiririka kuwa, hadi sasa (mapema wiki hii), Ivan hajakata tamaa, amekuwa akiendelea kumtongoza na kumuahidi ahadi mbalimbali.
Endapo atamkubalia na kuwa baby wake, basi atampa nyumba ya kifahari na magari ya kisasa (awe kama Zari).
Wema anakiri mwenyewe: “Alianza kuniahidi maisha mazuri, nyumba, magari na hata kunioa lakini kimsingi sijamkubalia kwani sijamwamini kama ana mapenzi ya dhati. Nahisi kuna kitu nyuma yake kinamsukuma kufanya hivyo.”
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa Wema akaingia kwenye himaya ya Ivan kutokana na ushawishi wake mkubwa anaoufanya kwa madam huyo, hivyo akawa tajiri mkubwa.
“Wema kwa sasa hatakiwi kuichezea bahati kwani Ivan ni mtu anayejiheshimu. Ana biashara zake kubwakubwa, hivyo suala la fedha za maisha hazimpigi chenga,” kilisema chanzo hicho. Akizungumzia suala hilo, rafiki wa karibu wa Wema ambaye hakupenda jina lake liandikwe , alisema licha ya Wema kutokubali ombi la Ivan lakini anaamini siku si nyingi atakubali na atakuwa vizuri kiuchumi kuliko alivyo sasa.
“Jamaa yupo serious na ndoa, Wema atakubali tu na ndoa itafungwa. Mtoto wa kike sasa atakuwa si wa magari ya kawaida, full kubadilisha, atakuwa mtamu kama mcharo,” alisema rafiki huyo.
Rafiki huyo aliendelea kusema kuwa, Wema ana wasiwasi kwamba, mapenzi ya Ivan kwake ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa sababu ya Diamond (aliyekuwa mpenzi wa Wema) sasa yuko na Zari (aliyekuwa mke wa Ivan).
“Kwa hiyo Wema ana wasiwasi kwamba, siku akimkubalia tu Ivan akapiga naye ngwara, biashara itakuwa imeishia hapo kwani nia ya kisasi ya mwanaume huyo itakuwa imekamilika,” alisema rafiki huyo.

Lady Jaydee atangaza mchongo huu kwa mashabiki wake

Lady Jaydee anataka kula dinner na mashabiki wake. Unachotakiwa kufanya ni kujirekodi na kupost video kwenye Instagram au Facebook ukiimba wimbo wake mpya, Ndindindi.
Lady Jaydee ameandika:
Katika watu wote waliotuma videos Wanaimba NdiNdiNdi Nawashukuru sana Wanaopenda kuendelea wanakaribishwa Ila nitakuwa nazi like huko huko Kwenye page zenu Kifuatacho sasa Nitachagua Clips 3 bora zilizokonga na kusuuza watu wengi Na watatu hao, nitafanya mchakato wa kula nao japo dinner Na ku hang nao siku yoyote nikiwa na event kubwa Majina nitataja baadae kidogo 1. 2. na 3.

Video MPYA: Kwenye video mpya za bongofleva ni hii mpya ya Amini ‘hawajui’

Kwa harakaharaka ni zaidi ya miezi kumi na mbili imepita toka mara ya mwisho nimetazama video mpya ambayo Amini yuko ndani, ni mwimbaji mwenye miaka yake kadhaa kwenye game ya bongofleva na sasa katuletea hii mpya, ukishamaliza kuitazama usisahau kumuandikia ajue watu wake wameipokeaje.

Rais Magufuli kaamua kutoa ofa ya vinywaji kwa watu wake Airport Mwanza…(+Pichaz)

Leo March 29 2016, kwa mara ya kwanza Rais Magufuli ametua kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza na kukutana na viongozi wa mkoa Mwanza pamoja wananchi wake waliokuwa Airport ya Mwanza, Kingine alichokifanya ni kwenda kwenye Mgahawa wa kawaida kabisa uliopo pembeni ya Airport nakutoa ofa ya vinywaji kwa wananchi wake wajumuike pamoja kwenye hiyo moments
 Rais Magufuli akitoka kuelea kwenye Mgahawa
Rais Magufuli akiongea na Meya wa Ilemela Renatus Mulunga na Meya wa Jiji James Bwire

Watu wakapita na ofa ya Rais Magufuli.
 Wanahabari nao wakapita kwenye ofa
 Rais Magufuli amepita Mwanza akielekea Chato nyumabani kwao kwa mapumziko ya siku tano na baada ya hapo ataanza ziara yake ya kikazi mkoa wa Mwanza.

Barakah da Prince ‘ajilipua’ kwa Naj


Msanii wa Bongo Fleva ‘Barakah da Prince’ akiwa na mpenzi wake Najma Dattan ‘Naj’. HATIMAYE! Baada ya kufichaficha kila sehemu juu ya uhusiano wao, msanii wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ ameamua ‘kujilipua’ kwa mpenzi wake mpya, Najma Dattan ‘Naj’ na kwamba ndiyo kila kitu kwake.
Akiliachia domo liserereke, Barakah anayebamba na Ngoma ya Siwezi alisema kuwa japokuwa amekuwa akifuatwa na vyombo vingi vya habari kujua ukweli sasa imefika wakati wa kutoa tamko.
“Ujue siku zote nilikuwa sijapata mtu sahihi katika maisha yangu. Nimempata Naj na naamini kwa asilimia zote ana maono ya mbele tofauti na wote niliowahi kuwa nao, pili tunaendana kwa kila kitu na mwisho ni mshauri wangu hivyo sioni sababu ya kuficha,” alisema Barakah.

Diamond Platnumz na Zari ndani ya mahaba mazito Sweden

 
Watakufanya utamani kupenda ukapendwa – maake kunakupenda usipendwe na badala yake ikawa tu karaha, mapenzi usiyafurahie tena. Lakini kwa Zari the Bosslady na Diamond Platnumz ni mahaba mazito kama ya Romeo and Juliet kwenye visa vya William Shakespeare. Wenyewe wanajiita Mr and Mrs Smith aka Brad Pitt na Angelina Jolie.
Mapenzi yao (ambayo walau yanadhihirika kwa picha zao za Instagram), yanaweza kuwapa wivu uliochanganyikana na hasira maex wao. Jioneee mwenyewe picha zao wakiwa backstage kabla ya hitmaker huyo wa ‘Make Me Sing’ hajapanda stejini huko Stockholm, Sweden. 


Tazama Video Jinsi Raila Odinga Alivyoanguka Jukwaani Wakati Akihutubia Wananchi Siku ya Pasaka....

Cord leader Raila Odinga is reportedly nursing injuries after he was injured during a recent trip to Mombasa County.
Odinga was addressing his supporters when a dais he was speaking on collapsed and leaders fell to the ground. 

Picha za WEMA SEPETU akiwa katika Instagram Party Jijini Mwanza

 
Usiku wa tarehe 27, ulipambwa na Show ya Instagram Party kwa upande wa Mwanza 88.1, mastaa kadhaa wa Tanzania walikuwepo kunogesha Party kutoka Bongo movie Wema Sepetu, alikuwepo na kundi la Weusi liliwakilishwa na Joh Makini pamoja G nako.Party imefanyika Rock City Shopping mall Mwanza.