Mrembo Amvamia Dully, akiona cha mtema kuni


Mrembo huyo baada ya kupanda jukwaani ili acheze na Dully.

DAR ES SALAAM: Hii ni aibu ya Pasaka! Mrembo mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, mwishoni mwa wiki alijikuta akifedheheka baada ya kushushwa jukwaani, alikoenda kwa lengo la kucheza pamoja na mkongwe Dully Sykes aliyekuwa akitoa burudani huko Sunrise, Kigamboni jijini Dar.
Akitolewa jukwaani hapo
Akiwa amevaa mavazi yaliyoonesha sehemu kubwa ya mwili wake, huku akionekana kuzidiwa na kiburudisho, mrembo huyo alikuwa akicheza kwa kukata kiuno hovyo kiasi cha kuwa kero kwa mashabiki wengine.
Ilikuwa majira saa 6 usiku baada ya wasanii kuanza kupanda jukwaani. Ishu kamili ilikuja baada ya Msaga Sumu kufungua shoo kisha wasanii wengine kuburudisha, ilipofika zamu ya Dully, mrembo huyo alikurupuka kutoka alikotoka na kupanda jukwaani kumvamia akiwa amevaa nguo zenye rangi iliyofanana na mwili. 

Akishushwa jukwaani mkuku.
Lakini kabla hajafanya lolote, mmoja wa vijana waliokuwa wameongozana na Dully, alimdhibiti mrembo huyo kwa kumshusha jukwaani. Kuonesha kuwa alikuwa ‘crezi’ na mkali huyo wa kibao cha Nyambizi, mrembo huyo aliendelea kucheza kwa furaha huku akishangilia kana kwamba hakukuwa na chochote kilichotokea.
Dully Sykes
Baadhi ya wasanii wakongwe waliokuwepo katika tamasha hilo lililoandaliwa na Promota Majid Bonga, baada ya kutimiza miaka 25 kama mdau wa sanaa ni pamoja na Juma Nature, Sister P, Manzese Crew, Zig Zag Crew, Solid Ground Family, Inspector Haroun, Afande Sele, Soggy Doggy, Mabaga Fresh, Dully Sykes, Jaffarai na wengine kibao


x

;

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »