Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi kugombea.
Akizungumza juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama hicho.
“Mimi siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona wenzanguwote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza kuchukua,” alisema Kajala.
;