Zari atumika kumdhalilisha Wema...Kisa kuzaa na Diamond Platnumz!


zarinah
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’

WATU wabaya! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia watu wanaoasadikiwa kuwa ni wafuasi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutumia jina na picha ya mwandani wa sasa wa staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumdhalilisha mpenzi wa zamani wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tangu Zari, ambaye ni mjasiriamali maarufu aliyemzalia Diamond, amfanyie mwanaye Latiffah ‘Tiffah’ sherehe ya kumtoa nje kwa mara ya kwanza (Arobaini).
ZARI (1)
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
KIINI CHA UDHALILISHAJI
‘Kirusi’ wa kwanza kuanzisha udhalilishaji huo alijitambulisha katika mtandao wa Instagram kwa jina la Who is Boss ambapo aliweka picha inayomuonyesha Zari akiwa amembeba mtoto wake na Wema akiwa amembeba mbwa kisha kusindikiza ujumbe uliosomeka:
“Ukibeba mimba utalea mtoto na ukitoa mimba utalea mbwa.”
TIMU DIAMOND ZAMSHAMBULIA WEMA
Mara baada ya Who is Boss kuweka picha na ujumbe huo, wafuasi wa Diamond (Team Diamond) walianza kumshambilia Wema kwa kumkejeli na kumtukana matusi mazito yasiyoandikika gazetini.
Wafuasi hao walimtuhumu Wema kuwa alichezea ujana kwa kutoa mimba matokeo yake kwa sasa analea mbwa wakati mwenzake Zari ametumia ujana wake vizuri na ndiyo maana amemzalia Diamond.
wema (3)
Wema Sepetu ‘Madam’.
WEMA ABUBUJIKWA MACHOZI
Chanzo kilicho karibu na Wema kilipenyeza habari kuwa alipopewa taarifa hizo za kudhalilishwa mtandaoni, alisikitishwa na kejeli hizo kiasi cha kumwaga machozi kwani suala la kutopata mimba yeye linamtesa hivyo mtu anapomkejeli, anaumia sana.
“Huwezi amini Wema amemwaga machozi. Anaumizwa sana na hawa watu wanaomkejeli kila kukicha mitandaoni hususan katika suala linalohusu mtoto,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambaye alikiri kukejeliwa na kusema ameumizwa na taarifa hizo hivyo analiomba jeshi la polisi nchini kuwashughulikia watu hao kupitia sheria mpya ya mtandao.
“Sijam-follow huyo mtu, ninapewa taarifa na watu, naamini atapatikana tu tena siku si nyingi maana watu wanapenda kutukana wenzao bila sababu za msingi,” alisema Wema.
MAMA WEMA ACHARUKA
Mbali na Wema, udhalilishaji huo ulimtibua mama mzazi wa staa huyo, Miriam Sepetu ambaye alisema hawezi kuacha suala hilo lipite hivihivi, atahakikisha ‘anadili’ na watu wote wanaomuandama mwanaye mitandaoni na kwa kuanzia watamshtaki Who is Boss.
“Hata siku moja sio haki kwa kweli, huwezi mtu ukasema kuwa analea mbwa na wakati hakuna hata mtu mmoja aliyempima mtoto wangu  na kujua hawezi kuzaa mtoto kwa hili sitokaa kimya nitamshtaki na piga ua, atapatikana tu,” alisema mama Wema.
AZIDI KUTIRIRIKA
Mama huyo alienda mbele zaidi na kusema kumekuwa na vitu vingi ambavyo vimekuwa vikimdhalilisha mwanaye na kumletea picha mbaya katika jamii, hivyo mamlaka zinazohusika na mitandao zinabidi zichukue hatua stahiki.
“Kwa hili sitanyamaza na itakuwa mfano maana watu wamezidi kudhalilisha   wenzao, TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) lazima ianze kufanya kazi yake na iwe fundisho,” aliweka nukta Mama Wema.

Chanzo: GPL



x

;

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »