ONA HII PICHA KALI YA MHE.MWIGULU NCHEMBA NA MWANAE ILIVYOZUA MJADALA MZITO MITANDAONI


Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimu ni ufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.

Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa,itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?

Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.

Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali


x

;

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »